Tuesday, 1 October 2019

VIONGOZI WA KIDINI WALALAMA JUU YA FILAM


Sheikh Abdallah Kundecha amesema nyimbo zinazoimbwa na wasanii wa kitanzania pamoja na Filam zinamzalilisha mwanamke pamoja na watoto kwani lugha zinazotumika kwenye nyimbo ni zamatusi pia wanawake katika filam wanatumika katika kuonesha maungo yao ya mwili ususani ni sehemu za sili huu ni udhalilishaji.

Nae mkurugenzi wa Bright Jamii Inshetive bibi Irene ambaye yupo kushoto wa Sheikh Abdallah Kundecha amevitaka vyombo vya habari na wasanii kupigavita maswala ya uzalilishaji wa wanawake na watoto kwa wandishi wa habari wasipige nyimbo za matusi na uzalilishaji na wasanii waache kutoa filam za kufedhehesha wanawake na watoto amesema haya Serena Hotel jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti inayohusu wasanii pamoja filam zipozalilisha wanawake na watoto.

habari picha na
Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment