Saturday, 26 October 2019

MKURUGENZI WA GLOBAL LINK EDUCATION ATETA NA WADAU


Abdulmariki mkurugenzi wa Global Link Education amewataka wadau wa sekta ya Elimu waendelee kuunga mkono tuzo zinazotolewa kwenye sekta ya Elimu hapa nchini.


Nae kwa upande Mwalimu Raurenti Ndoje anayefundisha shule ya sekondary ya Garanose ambayo ipo jijini Dar es Salaam Tegeta, Amewashukuru Global Link Education kwa kushirikiana na wizara ya Rais tamisemi na Serikali za mitaa kwa yeye kupewa tuzo ya kuwa mwalimu alikuwa amefanya vizuri katika kufundisha somo la Biology.


Suzan Hassani Bahati ni mwana aliyemaliza kidato cha sita Hasa Secondary School ambaye ni mshindi wa somo la History amewataka Global Link Education, Serikali na wadau wengine waendelee kutoa tuzo hizi za Elimu kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya ufaulu Nchini na kuwapa moyo na molali kufundisha zaidi Walimu.


Pichani waziri wa Ofisi ya Raisi na serikali za mitaa Selemani Jafu akimpa tuzo Mwalimu wa shule ya secondary ya Fedha kwa kufundisha vizuri kwa somo la Physics kitaifa kwenye tuzo za Global Link Education kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam huku Selemani Jafu akiwataka watunga miongozo wabadili mitaala ya Elimu kwani imekuwa ya kuwakomoa wanafunzi.

Pia akitaka tuzo hizi ziwe endelevu zi siwe za zima moto.

Habari Picha na 
Ally Thabiti 

No comments:

Post a Comment