Saturday, 26 October 2019

TBS YAWAFUNGULIA MILANGO WAJASILIAMALI WADOGO KATIKA KUELEKEA MASOKO YA KIMATAIFA.


Afsa mwandamizi wa shirika la viwango Tanzania TBS Joseph Ismail amesema wameamua kuwapa Elimu na mafunzo wajasiliamali wadogo kwenye Sekta ya usindikaji mazao ya kilimo na vipodozi lengo waweze kukizi viwango za bidhaa zao ili waweze kuuza hapa nchini na nje ya nchi amesema hawa wajasilia mali wadogo ni kundi ambalo limesaulika katika swala la kupewa Elimu juu ya bidhaa zao ndiyo maana tbs tumechukua maamuzi ya kuwafikia ili wakue kiuchumi na wawe na hali ya kutambua nao wanahusika kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza viwango za bidhaa zao za usindikaji na vipodozi na tbs inawatambua wajasilia mali wadogo kwa kuwapa elimu bule na huduma za viwango bila malipo.


Nae kwa upande wake Afsa viwango wa tbs kutoka idara ya kilimo na chakula Sanjo Noely Stephano amewataka wajasiliamali wadogo wa sekta ya mazao na vipodozi wazingatie matumizi ya viwango kwenye bidhaa zao kwani ni muhimu pia amefanua kuwa kunahaina mbili za viwango viwango vya lazima na si vyalazima ambako viwango vya lazima vinahasili mazingira,Afya ya mtumiaji na maswalaya uchumi ndiyo maana shilika la viwango bts linawataka wajasilia mali wadogo ili wazingatie viwango kwa maslahi ya biashara zao na Taifa.

Amemalizia kwa kusema faida ya matumizi ya viwango ikiwemo kuongezeka kwa masoko,kuleta imani kwa wateja na kukuza kipato cha mjasiliamali. amesema haya kwenye ofisi za Sido ambako shirika la viwango tanzania tbs lilipowafikia wajasilia mali wadogo wanaosindika mazao na anaotengeneza vipodozi vingunguti jijini Dar es Salaam.


Pichani wajasilia mali wadogo wakisikiliza kwa makini maada zinazo tolewa na wawezeshaji kutoka shirika la viwango Tanzania tbs kuhusu jinsi ya wajasiriamali hao wadogo kwenye sekta ya usindikaji wa mazao na bidhaa za vipodozi jinsi ya kuzingatia matumizi ya viwango ili wapate masoko makubwa semina hii imefanyika kwenye ukumbi wa sido jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na 
Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment