Thursday, 3 October 2019

WAZIRI WA KILIMO KUBURUTA MAHAKAMANI WATAKAO HUSIKA KUHUJUMU MBOLEA


Waziri wa Kilimo Japhet Asunga amsema bei elekezi za mbolea ni shilingi 45,000/= kwa mkoa wa Dar es Salaam na shilingi 58,000/= kwa Mkoa wa Rukwa amewataka wauzaji na wasambazaji wa mbolea wauze mbole zao nchini Tanzania kwa bei elekezi pia ni malufuku kuuza mbolea feki na wale watakao tolosha mbolea kupeleka nje ya nchi watachukuliwa hatua kali hikiwemo kupokonywa leseni zao na kufunguliwa mashtaka ya kuhujumu uchumi.

Amesema kifungu cha 4 sheria namba 9 ya mwaka 2009 na kanuni ya 56 ya mwaka 2011 inawataka makampuni ya mbolea kuhuza mbolea kutokana na bei elekezi iliyopangwa na serikali ametoa wito kwa watanzania kutumia vyama vya ushirika na TFRA katika kununua mbole na ametoa rai kwa mtu yeyote anaehitaji kuja kuwekeza ujenzi wa viwanda vya mbolea milango ipo wazi. Hata hivyo Japhet Asunga waziri wa Kilimo amewataka wakulima kutumia fursa za kpongua bei ya mbolea walime kwa wingi na watumie wataaramu kwa matumizi ya mbole.

Amesema haya jijini Dar es Salaam kwenye wizara ya kilimo wakatika akizungumza na wana habari.

Habari picha na
Victoria Stanslaus

No comments:

Post a Comment