Tuesday, 1 October 2019

SHIVIAWATA YATOA NENO KWA THRDC


Brandina Sembu katibu wa jumuhia ya wanawake na watoto shirikisho la vyama la watu wenye ulemavu (SHIVIAWATA) amesema kitendo cha THRDC kukusanya ripoti za maswala ya watu wenye ulemavu katika utekelezaji kupeleka umoja wa Mataifa ni jambo la kishujaa tena linatakiwa kuungwa mkono kwani serikali ya Tanzania kwa upande wa watu wenye ulemavu wanawake aiwatendei haki hata kidogo mfano walemavu wa kutosikia wakienda kujifungua mahospitalini hakuna wataaramu wa lugha za alama hivyo upelekea vifo vya watoto na mama wajawazito.
pia ni tatizo kwa vitanda vya kujifungulia kwa wanawake walemavu wa viungo vya miguu ambako vitanda hivi vipo juu zaidi hivyo amewataka THRDC kuwasilisha maswala haya ili yatendewe kazi huko umoja wa Mataifa ili serikali ya Tanzania iwajibishwe.

Habari picha na
Victoria Stanslaus 

No comments:

Post a Comment