Wednesday 28 August 2019

MAKONDA AWATANGAZIA NEEMA WANAUME WALIOTOSWA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Sala PaulMakonda amesema anapeleka maombi bungeni kuwepo na Sheria ya wanaume ambao walioahidiwa na wapenzi wao kuwa wakiwanunulia magali au kuwajengea nyumba za kifahari watawaoa baada ya kufanyiwa hivyo hao wanawake wanachukuwa hizo mali na kukataa kuolewa na hao wanaume hivyo ameliomba Bunge la Tanzania kutunga Sheria Dhidi ya wanawake wenye tabia hizi lengo kukomesha na kuondoa utaperi wa namna hii.
Amesema haya Jiji Dar es Salaam kwenye Ofisi yake wakati akiongea na wanahabari.
Habari picha na Ally Thabith

BODI YA FILAMU YATANGAZA VITA KALI


Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya filamu Dr. Kiagho amekamata CD ambazo hazina vibali na kutoa onyo kali kwa wote ambao wanasambaza CD ambazo hazina vibali kwani hatua kali zidi yao zitachukuliwa uku akisema kusambaza CD ambazo hazina vibali ni uhujumu uchumi kwani Serikali inapoteza mapato yake na uku wachache wakinufaika kama inavyoonekana pichani akiwa ameshikilia CD ambazo hazina vibali baada ya kubaini nakwenda kuzikamata. Ametoa wito kwa wananchi wa Wasanii wa Filam kutoa Taarifa pindi watakapo baini kuna watu hawalipi vibali vya CD kupitia bodi ya filamu.

Amesema haya Jiji Dar es Salaam kwenye ofisi ya bodi ya Filamu akiongea na wanahabari na akiambatana na viongozi wa Bodi ya Filamu.
Habari Picha na Ally Thabith 

ELIMU SOLUTION YALETA CHACHU NA MAPINDUZI MAZITO SEKTA YA ELIMU


Meithani Swedi mkurugenzi wa Elimu Solution amesema wameamua kutoa Tuzo kwenye Sekta ya Elimu lengo kuwamasisha wanafunzi wasome kwa bidii na waweze kufaulu kwa kiwango kikubwa kwenye Mitihani yao, Pia kuleta muamko kwa walimu wawe Molali na Juhudi za kufundisha na kuletha hamasa kwa wadau mbalimbali kutoa michango yao kwenye Sekta ya Elimu.
Mkurugenzi wa Elimu Solution amesema washiriki zaidi ya 70 watawania Tuzo za Elimu Award Tarehe 31/08/2019 viwanja vya mlimani city. Ambako mgeni Rasmi atakuwa waziri wa Serikali za mitaa Selemani Jafu Mkurugenzi wa LEmu Solution wanafunzi wenye ulemavu na walimu watapa tuzo kwa Juhudi walizozifanya na ufaulu waliouonyesha kwenye Elimu pia kutakuwa na zawadi kwa wilaya iliyofanya vizuri. Watanzania, Afrika Mashariki na kati na Afrika kwa ujumla ni mala ya kwanza Tuzo za Elimu zinatolewa Tanzania na Afrika kwa Ujumla
Amesema haya jijini Dar es Salaam kwenye Hotel ya Selena
Habari Picha na Ally Thabith

CATHERINE AWATAKA WADAU KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI





























Catherine Ndosi amewataka wadau mbalimbali wa muunge mkono Raisi Magufuli kwakuchangia Sekta ya Elimu Catherine Ndosi amewataka watanzania na wasio watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya mlimani city tarehe 31/08/2019 kwenye Elimu Awards ambazo tuzo hizi zitatolewa na Elimu Solution. Catherine Ndosi ameshukuru Kampuni ya ASAS, AZAM TV na COCACOLA kuwazamini na kufanikisha tuzo hizi,
Amesema haya jijini Dar es Salaam kwenye Hotel ya Selena.

Habari Picha na Ally Thabith

KAMPUNI YA ASAS YAIPA TANO TANZANIA ELIMU AWARDS


Abdul Twalib amesema wanaipongeza Taasisi ya Elimu Solution kwa kuandaa tuzo therasini na mbili kwa kategori 11 ambazo tuzo hizi zitatolewa tarehe 31/08/2019 katika ukumbi wa mlimani city.
Amesema kampuni ya ASAS inamiaka 19 katika biashara na usambazaji wa maziwa na bidhaa nyingine ambapo mpaka hivi sasa lita za maziwa laki tatu zimetolewa bure kwenye shule mbalimbali hapa nchini Tanzania na Kampuni ya ASAS lengo ni kuwafanya wanafunzi wapate Elimu bora na kuunga mkono juhudi za Rais magufuli kwakuelekea Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati.
Abdul Twalibu pichani akiwa kushoto ambaye ndio mzamini mkuu wa Elimu Awards kutoka kampuni ya ASAS amesema haya Jijini Dar es Salaam kwenye Hotel ya Selena.

Habari Picha na Ally Thabith

Tuesday 20 August 2019

Leah Mollel mshiriki wa maoenesho katika mkutano wa nchi jumuiya ya maendeleo kwa nchi za kusini mwa afrika SADC akizungumzia changamoto wanazokutana nazo watoto wa kiafrika na kusababisha kushindwa kuendelea na masomo sababu ya umbali wa shule na kulazimishwa kuolewa wakati wakiwa bado wadogo kiumri. Picha na ALLY THABITI

Moja ya washiriki wa maonesho ya nchi jumuiya ya SADC Kwa jina la Poges akiongelea changamoto wanazokabiliana vijana wanaopatikana kwenye nchi zinazounda jumuiya hiyo nakutoa pendekezo kuwa mkutano huo ulete tija ya kutatua changamoto hiyo ili vijana waendelee kujivunia kuishi kwenye mataifa yao nakuongeza uazalendo. Picha na ALLY THABITI

Mkurugenzi wa shirika la Oxfam Francis Odokorach akielezea namna shirika lao linavyoendelea kutoa elimu kwa wanawake ili waweze kujikwamua kiuchumi na kupambana na hali ngumu ya uchumi akitolea mfano kabila la wamasai ambao wamejitahidi kuwakwamua kielimu ili waweze kusimamia miradi yao na kupiga hatua za kimaendeleo? Picha na ALLY THABITI

VITENDO VYA UKATILI VIMEKITHIRI KWA ASILIMIA 66 KWA NUSU MWAKA 2019; LHRC

Mtafiti kutoka kituo cha sheria na haki za binaadamu Fundikiliza Zambi, akizungumza na waandishi wa habari kuelezea ripoti ya nusu mwaka inayooelezea hali ya ukatili kwa watoto ambao umeongezeka kwa asilimia 38 kwa maeneo ya kanda ya nyanda ya ziwa, ikifuatiwa na kanda ya nyanda ya juu kusini asilimia 32,kanda za kaskazini na pwani zimefungana kwa asilimia 9 wakati kanda ya kati ikiwa na vitendo hivyo kwa asilimia 7 na ya mwisho ni asilimia 5 ambayo imeshikiliwa na kanda ya magharibi. HABARI PICHA ; Ally Thabiti
mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binaadamu Bi Anna Henga, akitolea ufafanuzi ripoti ya nusu mwaka iliyotolewa leo Agost 20 mbele ya wanahabari jijini Dar es salaam, akisisitiza kuwa haki ya kuishi imeendelea kukiukwa sababu ya mauaji yanayotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi huku mengi yao yakitokana na imani za kishirikina, na kubainisha kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu watu wenye ulemavu wa ngozi wapo katika hatari ya kufanyiwa ukatili kwa sababu ya imani potofu dhidi ya viungo vyao. HABARI PICHA ; Ally Thabiti

Monday 19 August 2019

HALMASHAURI YA ILALA YAFANYA UCHAGUZI BILA MIZENGWE


Ojambi Dograsi Masabuli ameibuka kuwa naibu mea wa halmashauri ya Ilala kwa kupata kula 33 zidi ya mpinzani wake Eleni Liatura wa chama cha Chadema ambaye amepitwa kwa kishindo kikubwa kwa kuambulia kula 21.

Ambapo uchaguzi huu umekuwa wa kihistoria kwa Eleni Liatura wa chadema kukili kuwa uchaguzi ulikuwa wa huru na haki na amempongeza mgombea wa chama cha CCM kwa ushindi alioupata wa kuwa naibu mea wa halmashauri ya Ilala.

Naibu Mea Ojambi Masabuli amesema atawatetea wanyonge na atasimamia mapato yote ya halmashauri na ataisimamia miradi yote na hatapambana na vitendo ya rushwa. Uchaguzi huu umefanyika katika ukumbi wa Natogo ambako jumla ya wajumbe 57 wameuzulia na wajumbe amsini na nne wameweza kupiga kula.

Habari picha na 
Ally Thabiti.

DIWANI WA KIJICHI AWASHA MOTO KWA WAPINZANI

Diwani wa kata ya kijichi kupitia Chama cha Mapinduzi ccm Mtalawanje amesema wapinzani wasitegemee kuchukua nafasi za uwenyekiti wa Serikali za Mtaa kwenye Mitaa yote ya kijichi, Amesema haya kwnye mkutano wa hazara viwanja vya Mbaraka Mtaa wa Mgeni Nani ambako alikuwa anawaeleza wananchi Juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Chama cha mapinduzi CCM kwenye kata ya kijichi ikiwemo Sekta ya Afya, Elimu, Maji, Miundo mbinu, Mazingira na maswala ya ulinzi na usalamaambavyo vyote vimeimalika kwa kiasi kubwa pia amesema uwingi wa wananchi kwenye mkutano wake ni ushirikiano mkubwa wa serikali. Ametoa wito kwa wananchi wachangue mwenyekiti wa Serikali wenye uweredi na wasiopenda rushwa na wanaotoka chama cha mapinduzi
Habari Picha na Ally Thabit

Tuesday 6 August 2019

KAMANDA MAMBOSASA ATANGAZA VITA KALI KWA WAENDESHA BODABODA


Kama wa kanda maarum Dar es Salaam Razalo Mambosasa amewataka waendesha bodaboda kutofika mjini na bodaboda zao kipindihiki cha mkutano wa Sadeck lengo la kuwazuia kwakuwa waendesha bodaboda wanakaidi na kuvunja sheria za usalama barabarani na bodaboda zao pia wanatabia ya kuingilia misafara ya viongozi na kupita kwenye barabara za mwendo kasi.

amesema haya makao makuu ya jeshi la polisi kanda maarumu Dar es Salaam na agizo hili linatekelezw kuanzia leo tarehe 06/08/2019 na mwisho tarehe 18/08/2019 ambako jumla ya marais kumi na sita wanahuzulia mkutano wa 39 wa sadeck ambako rais magufuli anakabidhiwa wenyekiti wa Sadeck .

Habari Picha na
Ally Thabiti

Monday 5 August 2019

WAZIRI WA ELIMU AWAFUNDA VIJANA WA KISAYANSI WANAO CHIPUKIA


Prof Joyce Ndarichako waziri wa Elimu sayansi na Technolojia amewataka vijana wa kisayansi wanao chipukia waendeleze ujuzi walio upata kupitia YST na waende wakafundishe vijana wengine pia amewataka wanafunzi wa Chifu Dodo, Kisimili na Elboru wasibweteke kwa ushindi walioupata pia ameipongeza YST kwa kuwa na wazo mazuri kwa kuwamasisha vijana wa kisayansi wanao chipukia kuyapenda masomo ya sayansi na kuleta chachu kwa wengine pia amewataka YST uwongozi wake kuziangalia na shule za msingi pili kuwa na mwamko kwa wanafunzi wa shule za msingi kuyapenda masomo haya pia amewaambia serikali inaiyunga mkono YST kwa mchango wao na juhudi wanazozifanya kwa vijana wa kitanzania.

Ametoa wito kwa jamaii na taasisi mbalimbali kuwaunga mkono YST na shule mbalimbali ziwaunge mkono.

Habari Picha na
Ally Thabiti

MWENYEKITI WA YST ATABILI MAZITO


Prof Yunusi Mgaya mwenyekiti wa bodi ya YST amesema vijana wanao shiriki kwenye maonyesho ya ubunifu watafika mbali na amewataka wanasayansi vijana wanaochipukia wasikate tamaa kwani YST imekuja kwa malengo ya kuwaibua wanasayansi na kutatua changamoto zao huku akiipongeza serikali ya Rais Magufuli kwa kuwaunga mkono YST pia amezipongeza taasisi mbalimbali zilizojitolea kufadhili maonyesho ya wanasayansi wanochipukia

Nae mkurugenzi mtendaji wa YST Dr. Gozbert Kamugisha amemtoa ofu na mashaka waziri wa elimu na sayansi na technolojia Prof Joyce Darichako kuwa YST imezamilia kumuunga mkono Rais Magufuli katika kuelekea uchumi wa Viwanda kwa kuwatengeneza na kuwaendeleza vijana wa kisasa wanao chipukia na watazidi kutembelea mashule mbalimbali ili kuongeza kasi zaidi katika maonyesho haya ya wanasayansi wanaochipukia shule ya sekondari Chifu Dodo kutoka mkoa wa manyara imefanikiwa kupata namba moja kwa ubunifu wa Kisayansi wa kuwavuta nyuki na kupata ufadhili wa kwenda kusoma Afrika Kusini Alboru na Kisimiri imepata nafasi ya pili na ya Tatu.

Haya yamefanyika katika ukumbi wa mwalimu nyerere Posta jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

MWALIMU WA SHULE SEKONDARI YA IFAKALA AIPA TANO YST



John Samweli amesema mpango wa kuwainua wanasayansi vijana wa shule za sekondari ni mzuri kwani unawamasisha wanafunzi kupenda na kusoma masomo ya Sayansi amewataka viongozi wa YST wasikate tamaa na waongeze juhudi kuzifikia shule za msingi amesema haya kwenye maonyesho yaliaoandaliwa na YST kwa vijana wanasayansi wanaochipukia kutoka shule mbalimbaliza sekondari nchini Tanzania

Ambayo yamefanyika ukumbi wa mwalimu nyerere Posta jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

SHULE YA SEKONDARI IFAKARA YAAMUA KUTATUA CHANGAMOTO YA VYOO


Wanafunzi wa shule ya sekondari Ifakara wameamua kuamasisha jamii matumizi ya vyoo bora kwa wana Ifakara kupitia mradi wa nyumba ni choo.

Hayayamesemwa na mwanafunzi wa kidato cha Sita wa shule ya Sekondari Ifakara katika maazimisho ya wanasayansi wanaochipukia (YST) yamefanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.

Habari picha na '
Ally Thabiti