Diwani wa kata ya kijichi kupitia Chama cha Mapinduzi ccm Mtalawanje amesema wapinzani wasitegemee kuchukua nafasi za uwenyekiti wa Serikali za Mtaa kwenye Mitaa yote ya kijichi, Amesema haya kwnye mkutano wa hazara viwanja vya Mbaraka Mtaa wa Mgeni Nani ambako alikuwa anawaeleza wananchi Juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Chama cha mapinduzi CCM kwenye kata ya kijichi ikiwemo Sekta ya Afya, Elimu, Maji, Miundo mbinu, Mazingira na maswala ya ulinzi na usalamaambavyo vyote vimeimalika kwa kiasi kubwa pia amesema uwingi wa wananchi kwenye mkutano wake ni ushirikiano mkubwa wa serikali. Ametoa wito kwa wananchi wachangue mwenyekiti wa Serikali wenye uweredi na wasiopenda rushwa na wanaotoka chama cha mapinduzi
Habari Picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment