Monday, 5 August 2019

MWENYEKITI WA YST ATABILI MAZITO


Prof Yunusi Mgaya mwenyekiti wa bodi ya YST amesema vijana wanao shiriki kwenye maonyesho ya ubunifu watafika mbali na amewataka wanasayansi vijana wanaochipukia wasikate tamaa kwani YST imekuja kwa malengo ya kuwaibua wanasayansi na kutatua changamoto zao huku akiipongeza serikali ya Rais Magufuli kwa kuwaunga mkono YST pia amezipongeza taasisi mbalimbali zilizojitolea kufadhili maonyesho ya wanasayansi wanochipukia

Nae mkurugenzi mtendaji wa YST Dr. Gozbert Kamugisha amemtoa ofu na mashaka waziri wa elimu na sayansi na technolojia Prof Joyce Darichako kuwa YST imezamilia kumuunga mkono Rais Magufuli katika kuelekea uchumi wa Viwanda kwa kuwatengeneza na kuwaendeleza vijana wa kisasa wanao chipukia na watazidi kutembelea mashule mbalimbali ili kuongeza kasi zaidi katika maonyesho haya ya wanasayansi wanaochipukia shule ya sekondari Chifu Dodo kutoka mkoa wa manyara imefanikiwa kupata namba moja kwa ubunifu wa Kisayansi wa kuwavuta nyuki na kupata ufadhili wa kwenda kusoma Afrika Kusini Alboru na Kisimiri imepata nafasi ya pili na ya Tatu.

Haya yamefanyika katika ukumbi wa mwalimu nyerere Posta jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment