Wednesday, 28 August 2019
KAMPUNI YA ASAS YAIPA TANO TANZANIA ELIMU AWARDS
Abdul Twalib amesema wanaipongeza Taasisi ya Elimu Solution kwa kuandaa tuzo therasini na mbili kwa kategori 11 ambazo tuzo hizi zitatolewa tarehe 31/08/2019 katika ukumbi wa mlimani city.
Amesema kampuni ya ASAS inamiaka 19 katika biashara na usambazaji wa maziwa na bidhaa nyingine ambapo mpaka hivi sasa lita za maziwa laki tatu zimetolewa bure kwenye shule mbalimbali hapa nchini Tanzania na Kampuni ya ASAS lengo ni kuwafanya wanafunzi wapate Elimu bora na kuunga mkono juhudi za Rais magufuli kwakuelekea Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati.
Abdul Twalibu pichani akiwa kushoto ambaye ndio mzamini mkuu wa Elimu Awards kutoka kampuni ya ASAS amesema haya Jijini Dar es Salaam kwenye Hotel ya Selena.
Habari Picha na Ally Thabith
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment