Tuesday, 20 August 2019

VITENDO VYA UKATILI VIMEKITHIRI KWA ASILIMIA 66 KWA NUSU MWAKA 2019; LHRC

Mtafiti kutoka kituo cha sheria na haki za binaadamu Fundikiliza Zambi, akizungumza na waandishi wa habari kuelezea ripoti ya nusu mwaka inayooelezea hali ya ukatili kwa watoto ambao umeongezeka kwa asilimia 38 kwa maeneo ya kanda ya nyanda ya ziwa, ikifuatiwa na kanda ya nyanda ya juu kusini asilimia 32,kanda za kaskazini na pwani zimefungana kwa asilimia 9 wakati kanda ya kati ikiwa na vitendo hivyo kwa asilimia 7 na ya mwisho ni asilimia 5 ambayo imeshikiliwa na kanda ya magharibi. HABARI PICHA ; Ally Thabiti
mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binaadamu Bi Anna Henga, akitolea ufafanuzi ripoti ya nusu mwaka iliyotolewa leo Agost 20 mbele ya wanahabari jijini Dar es salaam, akisisitiza kuwa haki ya kuishi imeendelea kukiukwa sababu ya mauaji yanayotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi huku mengi yao yakitokana na imani za kishirikina, na kubainisha kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu watu wenye ulemavu wa ngozi wapo katika hatari ya kufanyiwa ukatili kwa sababu ya imani potofu dhidi ya viungo vyao. HABARI PICHA ; Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment