Shirika la viwango Tanzania TBS limepiga marufuku vipodozi vyovyote kutoka nje kuingizwa nchini bila kufanyiwa maombi kupitia njia ya mtandao ya tovuti ya anuani ya shirika hilo
Hatua hiyo ni mkakati wa TBS kutaka kuviifanyia uhakiki vipodozi vyote vinavyoingizwa nchini Kama ambavyo vimeruhusiwa kwa matumizi ya Tanzania ama la
Marufuku hiyo imetolewa na mkaguzi mwandamizi wa viwango TBS Donald Manyama wakati wa zoezi la ukamataji wa vipodozi vyenye viambata sumu linaloendelea kwenye maduka ya jumla na rejareja jijini Dar es Salaam.
Amesema kumekuwa na wimbi la uingizwaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku ambapo wafanyabiashara wengi wanadai wanapoagiza hawajui vimeruhusiwa ama lah hivyo uhakiki utasaidia kutoa taarifa ni vipodozi vipi vinarusiwa vipi haviruhusiwa.
Pia Donald Manyama Mkaguzi Mwandamizi TBS akaelezea walivyojipanga kukabiliana na wale wote wasio waaminifu watakapenyeza vipodozi hivyo kwa njia ya panya.
Yamesema haya na Donald manyama mkaguzj mwandamizi TBS.
Pichani maafisa wa TBS wakikagua vipodozi vyenye viambata vya sumu.
Habari Picha na
Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment