Friday, 8 November 2019

TAASISI YA UTAFITI YA AFYA YA IFAKALA YAJA NA MIKAKATI MIZITO YA KUTEKETEZA MALERIA


Mkurugenzi wa Taasisi ya afya ya Ifakala inayoshughulika na maswala ya utafiti wa Afya Tanzania Onorati Masanja wameamua kutoa chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano ili kupunguza vifo juu ya Maleria juu ya watoto hao pia wanatoa vyandalua kwa wamama wajawazito  bure ili kutokomeza vifo vya maleria kwa mama wajawazito na sasa wanafanya tafiti ya matumizi ya ndala pamoja na langi mbalimbali ambako itasaidia kuondoa maleria nchini.

Taasisi ya Utafiti ya Afya Ifakala inatawi Dar es salaam, Ifakala Mkoani Morogoro na Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Mkurugenzi amesisitiza kuwatafiti zao juu ya Maleria zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa ugonjwa wa Maleria nchini na kuokoa maisha ya watu wengi.

Amesema haya Mjini Bagamoyo kwenye semina ya wanahabari.  


Nae mwnahabari wa gazeti la mwananchi Lilian Timbuka kwa niaba ya wanahabari wote ameshukuru taasisi ya Utafiti ya Afya ya Ifakala kwa kuwapa mafunzo yanayousiana na maswala ya utafiti upande wa afya na namna ya kuandika habari za utafiti wa afya.

Lilian Timbuka ameitaka Taasisi ya utafiti ya afya ya Ifakala tafiti zao kuandika kwa lugha ya Kiswahili pia na amewahasa wanahabri mafunzo waliyoyapata wayatumie vizuri hii itawasaidia kuandika habari za afya kwa uweledi zaidi, ametoa wito kwa watafiti hapa nchini kutoa ushirikiano kwa wanahabari katika kutolea ufafanuzi maswala ya Afya.


Nae Dr. Shubis Kafuruki ambaye Principal Research kutoka taasisi ya utafiti wa afya ya Ifakala amewatoa ofu wanahabari kuwawakiitaji taarifa zozote kutoka taasisi ya afya ya Ifakala milango ipo wazi na wanakaribishwa amesema taasisi yao aifanyi tafiti kwa ugonjwa wa Maleria tu inafanya utafiti na ugonjwa wa HIV na magonjwa mengineyo ikiwemo TB.

Dr. Shibis Kafuruki amesema katika malengo yao matano kwenye utafiti maswala la kufanya semina na mafunzo kwa wanahabari ni moja ya malengo yao ivyo wameahidi kudumisha umoja, Ushirkiano na kuweka nguvu kwa pamoja katika maswala ya afya na wanahabari.

Amesema haya wakati akifunga semina kwa wanahabari mjini Bagamoyo kwenye mkoa wa Pwani kwenye Taasisi ya Afya ya Ifakala.


Pichani wanahabari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na Taasisi ya utafiti ya afya ya Ifakala mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Habari picha na 
Victoria Stanslaus 

No comments:

Post a Comment