Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wananchi kufanya uchunguzi wa awali wa kupima Saratani ya Matiti ili kujua hali zao na kupata matibabu mapema kwa wenye changamoto hiyo
Waziri Ummy ameyasema hayo Octoba Mosi, 2023 wakati akimuwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kwenye Maadhimisho ya Mwezi wa Saratani ya Matiti yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Saratani Ocean Road Jijini Dar es Salaam.
Waziri Ummy amesema Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa Saratani takribani Elfu Arobaini na Mbili (42,000) kila Mwaka ndio wanafika katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
Pia, Waziri Ummy amesema taarifa ya mwaka 2022/2023, inaonesha kuwa Taasisi ya Saratani Ocean Road ilihudumia wagonjwa wapya takriban 8,779 na asilimia 13 ya wagonjwa hao sawa na wagonjwa 1,141 walikuwa na Saratani ya Matiti.
Sambamba na hayo, Waziri Ummy amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wizara ya Afya kufunga mashine za CT-Scan katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na mashine za Ultrasound katika Hospitali zote za Halmashauri nchini.
Nae mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha matibabu kwa kutuletea vifaa tiba vya kutosha kwaajili ya uchunguzi wa Saratani mbalimbali ikiwamo PET-CT huku maahine ya Cyclotron ikiwepo kwaajili ya kuzalisha mionzi tiba itakayo tumika hapa kwenye Taasisi huku bakaa ikipangwa kupelekwa kwenye maeneo mengine kwaajili ya kusaidia watanzania wengine.
Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ifikapo mwezi wa kumia mabapo watu duniani kote huungana kupingana na ushambulizi wa aina yoyote wa Saratani hii huku ikiwasaidia wananchi waliokwisha athirika na ugonjwa huo kupata matibabu
No comments:
Post a Comment