WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muuungano na Mazingira, Seleman Jaffo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe mkoani Pwani, amekabidhi mifuko 600 ya sarufi kwa madiwani wa kata za wilaya hiyo kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Shikizi.
Aidha Waziri Jaffo ametoa mitungi ya gesi 126 kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya na mkoa ikiwa ni jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kutunza mazingira.
Waziri Jaffo amekabidhi mifuko ya saruji na mitungi ya gesi kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya kilichohudhuriwa na Katibu wa Chama hicho Mkoa Waziri Jaffo alisema lengo ni kuunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri.
Amesema tayari katika Jimbo la Kisarawe Shule zimejengwa katika maeneo mbalimbali na ni shule nzuri,ila kwa baadhi ya vitongoji bado hivyo wanaendelea na mchakato huo kuhakikisha kila kitongoji kinakuwa na shule shikizi.
“Leo nimetoa mifuko ya cement kwa shule 4 ambapo kila moja imepata matofali 150 yatasaidia kufyatulia matofali na kuanza ujenzi wa madarasa hata mawili mawili,”amesema na kuongeza
“Hii ni kuonesha Wananchi ni namna gani Chama cha Mapunduzi kinavyotekeleza ilani zake na kuhakikisha kila kitongoji kinapata shule hata vile vitongoji vya mbali kama cha Kimelemeta,”amesema.
Katika kikao hicho, hoja mbalimbali ziliibuliwa zenye lengo la kuboresha huduma kwa wananchi likiwemo suala la maji katika kata sita, Katibu wa CCM mkoa, Bernard Ghaty anatoa maelekezo.
Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Pwani,Bernard Ghaty amesema kipindi wanatoa ahadi katika ilani ya CCM waliwaambia Wananchi watadhibiti ukataji wa miti hovyo na kutengeneza mazingira ambayo ni Suluhu.
Alisema kwa vitendo Waziri Jaffo ameweza kutekeleza agizo hilo kwa kuhakikisha amegawa majiko ya gesi kwa watendaji wa CCM pamoja na wadau wengine ili wakawe mifano kwa watu wengine kuhakikisha wanatunza mazingira.
“Ni jambo la heshima,msingi na kuigwa kw akufata mfano wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha nchi inatunza mazingira na kuiga mfano wa Waziri Jaffo katika kuhakikisha
No comments:
Post a Comment