Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA Richard Kayombo amewatatka watanzania waanze kulipa kodi za majengo kuanzia sasa ili kuepusha usumbufu kama uliotokea mwaka jana,
Amesema hayo wakati wakutoa taarifa za makusanyo na mapato kwa mwaka 2017 kuanzia tarehe 1 mwezi 6 had mwenzi wa 12 ambapo ni trilioni 7.87 ikilinganishwa na sh trilioni 7.27 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha wa 2016/17 ambapo ni sawa na ukuaji wa asilimia 17.65
hata hivyo katika mwezi wa Desember pekee TRA ilikusanya jumla ya shilingi trilioni 1.66
aidha bwana Kayombo amewapongeza wafanyabiashara wenye makampuni na wananchi kwakulipa kodi pia amewataka wananchi wadai risiti na wafanyabiashara watoe Risit wanapouza bidhaa zao.
Habari Picha Na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment