Wednesday, 15 November 2023

RAISI WA ZANZIBAR AMEZITAKA NCHI ZA KIAFRIKA KUWEKA NGUVU KWA WANAWAKE

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi amewataka mawaziri wa fedha wa afrika kuweza kuwawezesha wanawake fedha ili waweze kujikwamua kiuchumi

Pia amewataka mawaziri wa Afrika wa wizara ya maendeleo ya jamii kuwatafutia wanawake fursa za uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi waondokane na maswala ya ukatili wa kijinsia huku wakizitaka nchi hizo kupitia kwenye mabunge yao kutenga bajeti wenye usawa wa kijinsia na kuweka sera bora kwaajili ya wanawake naye waziri wa Mwigulu Mchemba amesema kupitia mkutano huu Tanzania itajifunza namna ya kuwainua wanawake kiuchumi pia nitahamasisha nchi nyingine zitenge bajeti zenye usawa wa kijinsia kama ilivyo Tanzania kwaupande wake waziri wa maendeleo ya jamii Dr. Doris Gwajima amempongeza Rais Dr. Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwainua wanawake kiuchumi, watu wenye ulemavu vijana, wazee na makundi mengineyo na kwakuweza kutenga bajeti yenye mlengo wa kijinsia na kuwepo kwa sera na sheria rafiki kwa wanawake na makundi mengineyo.

habari kamili na Ally Thabit

No comments:

Post a Comment