Wednesday, 22 November 2023

WAKALA WA MAJENGO KUKUSANYA BILIONI 7.8

Mtendaji Mkuu  Daudi Kandolo wa Wakala wa Majengo Tanzania amesema tarehe 01/12/2023 watakusanya madeni kwa watumishi wanaoishi kwenye nyumba za wakala wa majengo ambao wanao daiwa kodi amesema kupitia kampuni ya Dalali ambako imepata mmlaka ya mahakama itakusanya madeni kwa watumishi wote ambao wamepanga na wanao daiwa kodi kwenye nyumba za TBA Tanzania nzima watakao shindwa kulipa watafukuzwa kwenye nyumba hizo na watapelekwa mahakamani ili waweze kulipa mikoa inayoongozwa kwa kudaiwa kodi na TBA Dodoma, Arusha na Mbeya.

Mtendaji Mkuu Daud Kandolo wa TBA amewataka wapangaji wote kutoa ushilikiano na zoezi hili litakuwa ndani ya mwezi mmoja ambako kiasi cha Bilioni 7.8 zitakusanywa na ile mikoa kinara inayodaiwa kodi Dodoma, Arusha na Mbeya itakusanywa Bilioni 1.4.

Habari na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment