Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Kiongozi Mkuu wa Chama hicho, Zitto Kabwe leo April 10 kimechambua ripoti ya CAG ambapo pamoja na mambo mengine kimeitaka Serikali kuheshimu Bunge na kufuata sheria ya Bajeti
Akiongea na Waandishi wa Habari, Dar es salaam leo, Zitto Kabwe amenukuliwa akisema “CAG amefanya ukaguzi wa Akaunti ya Deni la Taifa na kueleza kwamba hadi Juni 30, 2022 lilikuwa Shilingi trilioni 71 ambapo ni ongezeko la 11% kutoka deni la shilingi trilioni 64.5 lililo ripotiwa mwaka 2020/21”
“Uchambuzi wetu unaotokana na Ripoti ya CAG unaonesha kuwa katika mwaka huu wa ukaguzi Serikali ilichukua mikopo ya ndani kwa 30% zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano”
“Vilevile mikopo ya nje yenye masharti nafuu iliyochukuliwa na Serikali ilikuwa 33% zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge, mwenendo huu unaonesha Serikali kutojali na kudharau Mamlaka ya Bunge, tunaitaka Serikali kuheshimu Bunge na kufuata sheria ya Bajeti”
HABARI PICHA NA
ALLY THABITI
No comments:
Post a Comment