Tuesday, 24 August 2021

NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI AWA NA MATUMAINI NA KAIZEN

 William Olenasha Naibu Waziri wa Uwekezaji Tanzania amevitaka Sekta binausi nchini Tanzania watumie fursa zinazopatikana kwenye mradi wa KAIZEN Pia amewataka watanzania kutumia mradi wa KAIZEN kwani wataweza kujikwamuwa kiuchumi  na wataweza kupata Ujuzi wa Aina mbalimbali . 

Naibu Waziri wa Uwekezaji amesema serikali inafanya mabadiliko ya Sera na Sheria Lengo kuendana na uendeshaji na mradi guy wa KAIZEN ili kusiwe na mkwamo katika uendeshaji mradi wa KAIZEN. 

Nae Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke  Joketi Mwengelo ameapongeza nchi yaJapani Kwa kuleta mradi waKAIZEN kwani utaleta chachu ya kukuwa Uchumi Kwa watanzania na nchi ya Tanzania  amewataka watanzania kuchangamkia fursa hii.

Huku akiwataka vijana kuto kata tamaa.

Nae Jeni Liatuu kiongozi wa mradi wa KAIZEN  amesema watamfikia kila mtanzania Lengo Kuwajenga uwezo na kuwapa maarifa ya namna ya kujikwamuwa kiuchumi na kuondokana na umasikini .amesema haya jijini Dsm.

Habari na Ally Thabit

No comments:

Post a Comment