Saturday, 30 June 2018
TFDA YAMSHIKILIA ALIYESAMBAZA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI KUHUSIANA NA DAWA YA PANADOL
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Agnes Sitta Kijo amekanusha taarifa hizo za kwamba dawa ya panadol ukiimwagia maji inageuka kuwa kitambaa si zakweli, kwani dawa ya panadol ni salama kwa matumizi kama dawa nyingine.
Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo wa Mamlaka ya Chakula na Dawa amesema kuwa bidhaa inayohusishwa na dawa tajwa ni kitambaa (tab towel) ambacho kimetengenezwa kwa muundo wa kidonge na juu hakuna lebo ya Panadol wala paracetamol kam inavyoelezwa na katika video inayosambazwa, na badhaa hii hutumika zaidi katika mahoteli au maeneo mengine.
Habari picha na ALLY THABIT
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment