Tuesday, 10 July 2018

MHADHILI WA CHUO CHA KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE AWEKA MAMBO HADHARANI

Dkt Fillip Daninga ambaye ni mhadhili wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya mwalimu  nyerere amesema kuwa "lengo la luanzishwa kwa chuo hiki kuandaa vijana kuongoza nchi hii baada ya kupata uhuru wa Tanganyika ambapo waliweza kufundishwa na mpaka sasa wanafundisha maswala ya maadili,uadilifu,nidhamu,siasa na uchumi ili kuweza kupata viongozi bora ambapo lengo hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa"

Dkt Fillip Daninga akizungumza na mwanahabari katika maonyesho ya 42 ya biashara sabasaba Dar es salaam
Pia vilevile hakusita kutaja baadhi ya viongozi nguli ambao walinufaika na elimu hiyo akiwemo raisi mstaafu wa awamu ya nne mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,Mzee Kaduma,Mzee Fillip Mangula,mh Nape Nauye ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama Lindi na mh Isaya Mwita ambaye ni meya wa jiji la Dar Es Salaam
Hakusita kusema jinsi chuo kinavyo wafikia jamii kwa njia ya makongamano,matangazo ya radio na televisheni, kwa machapisho mbalimbali kwa njia ya vitabu,majarida na kielectronic pia wamejipanga kutoa elimu ya ngazi ya juu masters, amesemahayo kwenye maonyesho ya biashara 42 sabasaba Dar Es Salaam.habari picha na Ally Thabit

No comments:

Post a Comment