Wednesday, 12 May 2021

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATOA NENO


 Prof Kitila Mkumbo Waziri wa Viwanda na Biashara amewataka makampuni ya Kitanzania,wafanya Biashara,wenye Viwanda na wajasilia mali wadogo wajitokeze kwa wingi kwenye maonyesho ya sabasaba ya 45 yatakayo fanyika Dsm .

Ambako watapata fursa mbalimbali kukuza bidhaa zao ,kutangaza bidhaa zao na kutambulika kitaifa na kimataifa .

Pia wataweza kubadilishana ujuzi na uzoefu kwenye Biashara, nchi zipatazo 7 zitaahiriki kwenye maonyesho ya sabasaba ,kampuni 54 kutoka nje ya nchi nazo zitakuwepo .

Huku kampuni  Kitanzania 2801 zitaahiriki .pia kutakuwa na mikutano ya B to B amesema haya jijini Dsm  makao makuu ya NDC wakati akiongea na Wana habari.

Habari picha na Victoria Stanslaus

No comments:

Post a Comment