Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema Treni ya Mwendokasi inatarajia kuanza safari kwa kipande kilichokamilika mwishoni mwa mwezi April au mwazoni mwa mwezi May mwaka huu.
Kadogosa amesema hilo Jijini Dodoma mara baada ya kuwasili kwa msafara wa Wajumbe wa Baraza Kuu la Wanawake wa CCM waliotumia usafiri wa Treni ya Mkandarasi kutokea Dar es salaam hadi Dodoma ili kushuhudia mwenendo wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR).
Kadogosa amesema “Hatutapandisha kwanza Abiria kuna matakwa ya kisheria ambayo tunafuata LATRA ambao wanatakiwa wafanye ukaguzi wao wakishajiridhisha kwenye mifumo tutweza kuanza, pia tuna suala la bei ambalo wanashirikisha Wananchi sehemu mbalimbali tunapofika”
No comments:
Post a Comment