Thursday, 2 March 2023

MAELEZO YA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI YA MHE. MKUU WA MKOA WA DSM KWA NIABA YA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZIJUU YA TUKIO LA SHUGHULI YA KUFUNGA MRADI WA MAJARIBIO WA MPANGO WA HATUA KUMI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA SALAMA NCHINI TANZANIA

 

MAELEZO YA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

YA MHE. MKUU WA MKOA WA DSM KWA NIABA YA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZIJUU
 YA TUKIO LA SHUGHULI YA KUFUNGA MRADI WA MAJARIBIO WA MPANGO WA 
HATUA KUMI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA SALAMA NCHINI TANZANIA

Tarehe 2 Machi, 2023

 

Habari za asubuhi kwenu nyote.

 

v Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa taasisi zilizofanikisha Mradi huu kwa Tanzania, ambazo ni:

                   i.            Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usalama Barabarani, UK Aid, na Global Road Safety Facility ya Benki ya Dunia kwa ufadhili wa Mpango huu.

                 ii.            Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika (UNECA) kwa kuwa taasisi ya Umoja wa Mataifa inayotekeleza mradi huo.

              iii.            Shirikisho la Barabara la Kimataifa (IRF) ambalo makao makuu yake yako Geneva, Uswizi kwa kuwa kiongozi wa mradi, na Mpango wa Kimataifa wa Tathmini ya Barabara (iRAP), Chama cha Barabara Duniani (PIARC) na Chama cha Barabara Tanzania (TARA) kwa kufanya kazi kama taasisi washirikakatika utekelezaji wa mradi huu hapa nchini Tanzania.

 

Pongezi zangu pia ziwaendee wadau wote kwa kuhusika kikamilifu katika mradi huu ambao umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kabisa duniani kutekeleza Mradi wa Majaribio wa Mpango wa Hatua Kumi wa Miundombinu ya Barabara Salama nchini Tanzania. Tunajisikia fahari kupata fursa hii na kwa matokeo ambayo miezi hii 30 ya kazi ya pamoja imeleta. Leo tupo kusherehekea kwa pamoja mafanikio haya ambayo utekelezaji wake utasaidia kuifanya nchi yetu kuondokana na barabara hatarishi.

 

v Ripoti ya Hali ya Kimataifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu Usalama Barabarani ya mwaka 2018 inakadiria kuwa zaidi ya watu 16,000 huuawa kwenye barabara za Tanzania kila mwaka. Vifo vingi huwa ni vijana. Usalama barabarani ndio chanzo kikuu cha vifo vya watoto na vijana wenye umri wa miaka 5-29.

Tumepewa dhamana na watanzania na hivyo tunalazimika kuchukua hatua na kubadili mwelekeo huu na Mradi wa Hatua Kumi umetupatia maarifa, ujuzi na zana za kufanya hivyo.

 

Septemba mwaka 2022tulikuwa na uzinduzi wa Programu ya Kitaifa ya Kutathmini Viwango na Usalama wa Barabara Tanzania (TanRAP) ambayo inaipatia nchi yetu jukwaa la kubadilishana na kujifunza kutoka kwa mataifa mengine, kupitisha viwango vya kimataifa vya ubora wa usalama wa barabara zetu kwa kuzipatia madaraja ya nyota 3 au zaidi kwa watumiaji wote wa barabara na kujenga uwezo na maarifa ya ndani kwa nchi yetu kwa siku zijazo.

 

Leo, shukrani pia kwa mradi huu wa Hatua Kumi, karibu Km 10,000 za barabara na miundo zimefanyiwa tathmini kupitia mbinu za iRAP ili kubaini usalama uliojengwa ndani ya barabara zote zilizopo na barabara zinazopendekezwa kuboreshwa. Tathmini hizo zimethibitisha kuwa hatua za usalama barabarani zitapunguza hatari za vifo barabarani na kuwa na faida kubwa kwenye uwekezaji.

 

v Makadirio ya gharama ya kila mwaka ya vifo na majeraha makubwa nchini Tanzania hugharimu dola za Marekani bilioni 4.1 sawa na asilimia 8.2 ya Pato la Taifa. Kwa hiyo, Ajali za barabarani zinawakilisha changamoto kubwa kwa Tanzania ambayo inahitaji mikakati na mipango ya kutosha.

Kupitia Mradi wa Hatua Kumi, wadau wengi  wamekuwa wakifanya kazi kwa muda katika kuandaa rasimu ya mapendekezo ya mkakati mahususi wa usalama wa miundombinu ya barabara na mpango kazi na ninayofuraha kushuhudia leo matunda ya kazi hiyo ambayo yataarifu hatua ya serikali tunapoandaa mkakati wa jumla wa usalama barabarani kwa nchi na tunapoandaa mipango ya uwekezaji wa barabarani. Mpango ulioandaliwa katika mfumo wa Mradi wa Hatua kumi unawasilisha mkakati wa kitaifa wa usalama wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania kwa kipindi cha 2021-2030. Mpango wa utekelezaji unalenga kutoa maendeleo, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya hatua za usalama. Kama ilivyoripotiwa katika ripoti, uwekezaji wa takriban 0.15% wa pato la Taifa (GDP) kwa mwaka hadi kufikia 2030 utakuwa umewezesha kwa kiwango kikubwa kuokoa maisha ya watu 7,100 kwa mwaka na pia USD 26 ya faida itapatikana kwa kila USD 1 itakayowekezwa.

v Ingawa hatua nyingi zinazohitajika ili kuokoa maisha ni rahisi kitaalamu na ni rahisi kujenga, kuna vikwazo vingi vya kufikia na kudumisha matokeo ya usalama barabarani nchini Tanzania. Viwango vilivyopitwa na wakati, na miongozo ni sehemu ya vikwazo hivyo. Tunashukuru kwa juhudi ambazo zimefanywa na wengi wenu katika kuandaa rasimu ya mapendekezo ya marekebisho ya Mwongozo wa Usanifu wa Kijiometri wa Barabara Tanzania (RGDM) ili kutathmini ufaafu wake katika kushughulikia mahitaji ya usalama wa watumiaji wote wa barabara na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UNSDG) namba 3 na 4 kwa usalama wa barabara mpya na zilizopo.

 

 

v Maarifa, ujuzi na ufahamu wa uhandisi usalama barabarani bado ni mdogo kati ya wataalamu wa usafiri katika nchi yetu. Nimefurahishwa kujua kwamba shughuli za kujenga uwezo wa Mradi wa Hatua Kumi kwa ujumla zimefikia zaidi ya wataalamu 500 wa Kitanzania na kwamba sasa tunaweza kutegemea wataalamu 150 ambao kupitia kozi za Mradi wa Hatua Kumi wamethibitishwa katika Uhandisi wa Usalama Barabarani. Tathmini za iRAP, Ukadiriaji wa Nyota wa Miundo na Ukaguzi wa Usalama Barabarani.

 

Tumepanga kuweka ari na kasi sawa, kutoa mafunzo kwa watu wengi zaidi na kufanya maendeleo kwa nchi yetu na watu wetu kupitia mpango wa kitaifa wa mafunzo na ithibati kama ilivyoandaliwa na Mradi wa Hatua Kumi kufuatia mapitio ya kina ya mafunzo yaliyopo na tathmini ya mapungufu ya mafunzo.

 

 

Sasa tuendelee na kazi nzuri na tuifanye kwa pamoja Tanzania bila barabara hatarishi!

 

Ahsanteni Sana.

 

No comments:

Post a Comment