Mkurugenzi wa mikakati ,Benjamini Mpamo kutoka selcom ameongezea kwa kusema,dhamira kuu ya selcom ni kuwarahisishia maisha watanzania kwa njia ya teknolojia na kuakikisha huduma za kifedha zinapatikana kwa njia rais na haraka kwa watanzania wote.katika kuhakikisha wanatimiza dhamira hii, selcom kwa kushilikiana na Exim benki wamewaletea huduma hii ya Cashpoint Atm ili kuwawezesha watanzania kutoa fedha kiuraisi kabisa muda wote inapohitajika .huduma zingine zinapatikana kwenye Cashpoint Atm hivi karibuni ni pamoja na kununua Luku,kulipia bili ya maji[ Dawasco], kununua muda wa maongezi, kuangalia salio na kupata taarifa fupi ya miamara ya kadi kwa wateja wa Visa na Master Card. lengo kuu la Cashpoint Atm ni kuwaraisishia wananchi huduma za kutoa fedha na kuwawezesha kutoa fedha muda wowote kwa haraka,salama na uhakika bila kuwa na wasiwasi wa kukosa huduma hii
habari picha na ALLY THABITI
No comments:
Post a Comment