Prof Charles D.Kihampa Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania amesema Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU inapenda kuwafahamisha Umma na Wadau wa Elimu ya Juu nchini kuwa Udahili katika awamu zote tatu Kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika taasisi za elimu ya Juu nchini Kwa mwaka wa masomo2021/2022 umekamilika Kwa mujibu wa ratiba ya Udahili iliyoidhinishwa na Tume.
Kufunguliwa Kwa Awamu ya Nne ya Udahili Baada ya kukamilika Kwa Awamu zote tatu za Udahili,Tume imepokea maombi ya kuongeza muda WA Udahili kutokana na sababu mbalimbali .
Pia Time imepokea maombi ya kuongeza muda WA udahilikutoka Kwa baadhi ya taasisi za elimu ya Juu nchini ambazo bado zina nafasi katika baadhi ya programs za Masoko Kwa mwaka 2021/2022.
Ili kutoa fursa Kwa waimbaji ambao hawakuweza kudahiliwa au kuweza kuomba Udahili katika awamu tatu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali , Tume umeongeza muda wa Udahili Kwa kufunguka Awamu ya Nne na ya mwisho ya Udahili inayoanza Leo tarehe 11 Oktoba Hadi 15 Oktoba 2021/2022. Tume inawaasa waimbaji wote watumie fursa hii vizuri ili kupata nafasi ya Udahili.
Tume imetoa Rai Kwa waimbaji wa Udahili na Vyuo kuzingatia utaratibu wa Udahili katika awamu ya Nne .
Habari picha na Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment