Damask Ndumbalo Waziri wa Maliasili na Utalii anamshukuru raisi Samia Suluhu Hassan Kwa kuipa Wizara yake Fedha za Kitanzania bilioni 29 Kwaajili ya Kupambana na UVIKO 19.
Waziri Ndumbalo amesema Fedha hizi zitatumika kwenye miradi 5 mfano kutoa elimu Kwa waongoza Utalii,kutengeneza vipeperushi na mabango.
Pia amesema fedha hizi zitatumika kwenye Mikoa 26 Tanzania bara, ametoa onyo Kwa watakaoiba fedha hizi hatua Kali zitachukuliwa dhidi Yao ikiwemo kufukuzwa kazi na kupelekwa mahakamani.
Habari picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment