Monday, 25 January 2021

WHO YALIA NA UKEKETAJI

kila ifikapo tarehe 6 mwezi pili ni siku ya kupinga ukeketaji ambako maswala makubwa yatokea baada ya mtoto wa kike kukeketwa ikiwemo kutokwa na damu nyingi na kupelekea kifo kwa mkeketwaji pia wakati wakujifungua mzazi hufa au kiumbe kinachozaliwa hufariki ndio maana WHO imekuja na mpango mikakati ya GVV lengo kutokomeza maswala ya ukeketaji Tanzani, Afrika na ulimwenguni kwa ujumla

kwa mwaka zaidi ya mamilioni ya wakeketwaji hufariki na wengine wanabaki na makovu shinyanga na mikoa mingine ni vinara katika maswala ya ukeketaji. WHO imetoa wito kwa watanzania na ulimwengu kwa ujumla kupinga na kutokomeza mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Habari picha na Ally Thabith

TAKUKURU YATEMA CHECHE



Mkuu wa Takukuru wa Temeke Ndugu Kessy amesema watu watoe taarifa zinazohusiana na maswala ya kuombwa rushwa au zakutoa rushwa kupia namba 113  lengo katika huduma mbalimbali zitolewe kwa haki bila uonevu wameweza kuokoa kiasi cha Shilingi milioni ishirini na tatu na zaidi wamesimamia kesi nne mbili wameshinda na wanasimamia miradi yenye thamani ya bilioni therathini na saba huku wakianzisha virabu mbalimbali vyakupinga rushwa.

Habari Picha na Ally Thabith

 KAMISHINA MSAIDIZI WA USALAMA BARABARANI AINISHA MIKAKATI MIZITO

Ndugu Mutafungwa Kamishina Msaidizi wa Barabarani amesema wamejipanga katika kuzibiti ajali barabarani kwa kuwachukulia hatua kali wale wote wasiofuata kanuni, Sheria na utaratibu wa sheria barabarani ndugu mtafungwa amepongeza shirika la afya duniani WHO kwakuisaidia serikali ya Tanzania dhidi ya mapambano ya kudhibiti ajali za barabarani kwa kuja na mradi wa kutoa elimu kwa wanahabari jinsi ya kuandika maswala ya barabarani pamoja na kuwapa elimu wanasheria amesema haya kwenye semina iliyowahusisha wanahabari Jijini Dar es Salaam nayo wizara ya Afya wamesema ajali barabarani zikipungua nchini zitasaidia kupunguza vifo kwa wingi na gharama za kuwatibu waga wa ajali zitatumika kwenye maendeleo ya nchi nao WHO wamawataka wanahabari kupaza sauti zao na watumie karamu zao vizuri ili ajali zisitokee nchini Tanzania.

Penina ni mwanahabari kutoka gazeti la majira kwa niaba ya wanahabari wenzake ameipongeza serikali, jeshi la polisi pamoja na WHO kwa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo jinsi ya kuandika habari za barabarani.

Habari na Ally Thabith

Monday, 18 January 2021

RAIS AVALIA NJUGA MIGOGORO YA NDOA

 Aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia chama cha Chadema DKT. MAYROSE KAVURA MAJINGE ameamua kuanzisha taasisi ya kushughulikia matatizo ya wanandoa pamoja na wachumba ambayo inaitwa The family is the firts assential cell of human society " tafsiri yake ni kuwa "Familia ni chembe muhimu ya kwanza ya jamii ya binadamu" amesema migogoro ya ndoa inazolotesha uchumi wa mtu na Taifa na ufanisi wa kazi unapotea.

Hivyo taasisi hii itakuja kuwa mwarubaini wa matatizo haya ambako watatoa elimu ya sili pamoja video tarehe 20/01/2021 taasisi hii itazinduliwa msimbazi centre saa 12:00 jioni wote munakaribishwa bila kiingilio.

Habari na Ally Thabiti

Sunday, 17 January 2021

 


JATU PLC YAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFURI

meneja wa JATU PLC SIMBA SINGANO amesema kuwa wamekuja na programu ya kuwafikia wanafunzi wa vyuo lengo waweze kujiajili kwenye kilimo ambako asilimia 50 ya ajira zilizopo nchini zinatokana na kilimo program ya UNI TALK ikaibua fursa mbalimbali hapa nchini na lengo ni kumuunga mkono raisi magufuri kwa kutekeleza hilani chama cha mapinduzi kwa kuzalisha ajira mbalimbali ndio maana JATU PLC imeingia mkataba na MISS TANZANIA wa mwaka 2018 ili awe balozi wa JATU PLC kwa mwaka mmoja nae balozi wa Jatu ambae Elizabeth Miss Tanzania 2018 amewatoa mchecheto watanzania kuwa kilimo kinaweza kuwakwamua kiuchumi huku akiahidi kuwa atakuwa balozi mzuri na atatembelea vyuo vyote kumi na watu wenye ulemavu watafikiwa kwa kiwango kikubwa.


Habari na Ally Thabith

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATOA MAAGIZO MAZITO

Jofrey Mwambe waziri wa viwanda na biashara amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa wakala na vipimo STELA KAWA kusimamia na kufuatilia vipimo vya bidhaa kwenye viwanda kwani ujazo na urefu wa bidhaa hizo si sahihi kwani hii itafanya viwanda vyetu vife nae kaimu Mkurugenzi wa wakala wa vipimo Tanzania Stela Kawa amesema maagizo yote aliyotoa waziri atasimamia na kufuatlia kwaajili ya kunusuru viwanada vyetu huku akiwataka wenye viwanda kuzingatia sheria, kanuani na taratibu za vipimo kwenye bidhaa zao na atakaeshindwa saheria kali itachukuliwa dhidi yake.

Habari na Ally Thabith


 

NCCR MAGEUZI YAWASHA MOTO

Mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI James Mbatia amemtaka Rais Magufuri kuendeleza mchakato wa katiba mpya huku akisema tume ya Taifa ya uchaguzi hawajatenda haki kwa vyama vya upinzani.

Habari picha na Ally Thabith


 BARAZA LA MITIHANI LAPONGEZA 

katibu mtendaji wa baraza la mitihani Dr. Charles Msombe amesema ufaulu wa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 5.19 kwa kidato cha nne hivyo amewapongeza wanafunzi, walimu, wazazi na walezi, pamoja na walimu wakuu kwa kuweza kuwasimamia vijana wao huku baraza likiwafutia matokeo wanafunzi 215 kwa udanganyifu.

Habari picha na Ally Thabith

MKURUGENZI WA TBS AMEAHIDI MAZITO

Yusuph Othaman Ngenya Mkurugenzi mkuu wa TBS amemwambia waziri wa viwanda na biashara Geofrey Mwambe kuwa yeye na watendaji wengine wa TBS wanatekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo yanayotolewa na waziri GEOFREY MWAMBE pia amewatoa hofu wajasilia mali wadogowadogo kuwa milango ya tbs iko wazi.

Habari na Ally Thabith

 


WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATOA NENO KWA TBS

Jofery Mwambe waziri wa viwanda na biashara ameutaka uongozi wa TBS kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogowadogo na kupunguza muda wa kutoa vibali kutoka miezi sita (6) mpaka miezi mitatu (3) na vile vya mwaka bila kupunguza pia Tbs itengez biashara kwa watanzania. Amesema haya alivyofanya ziara makao makuu ya TBS kama inavyoonekana pichani akiwa na ndani ya Maabara za TBS jijini Dar es Salaam.

Habari picha na Ally Thabith 

Thursday, 7 January 2021

GOBA MARASONI KUNUSURU VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO

 Mwenyekiti wa mbio za Goba Marasoni Benson Luwoga ameishukuru NIC kwa kuifadhili miaka mitatu Goba Marasoni kwani ufadhili wao utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii ambako fedha za mwaka huu zitakazo patikana kupitia Goba Marasoni zitakwenda kupunguza vifo vya Wamama Wajawazito na Watoto wakati wa kujifungua. 

Ambako kauli mbihu mwaka huu inasema kimbia kwa kuboresha maisha ya mama na mtoto ambako tarehe 30/01/.2021 kutakuwepo na mbio za Goba Marasoni ambako washiriki watakuwa 2000 pia mbio hizi zinasaidia watu kuimarisha afya zao na kuepukana na marazi nyemerezi yasio ambukiza Mfano Kisukari.

Benson Luwoga ametoa wito kwa taasisi na wadau wengine kujitokeza kwa wingi kuzamini mbio hizi za Goba Marasoni

Habari Picha na 

Ally Thabiti

NIC YAMWAGA MAPESA KWA GOBA MARASONI


Mkurugenzi wa shirika la Bima nchini Tanzania (NIC) Elirehema Doriye asema wameamua kuwa wazamini wa mda wa miaka mitatu kwenye goba marasoni rengo kuunga mkono juhudi za Raisi Magufuli na kutekeleza ibara ya Nane ya chama cha Mapiduzi katika kukuza ajila kwa vijana amesema wameanza kutoa kiasi cha Shilingi Milioni Ishirini na Tano (Tsh. 25,000,000/=)  kwa mwaka huu mmoja ila kiwango cha pesa kitazidi kukuwa kila mwaka 

 

Habari Picha na 
Ally Thabiti