KAMISHINA MSAIDIZI WA USALAMA BARABARANI AINISHA MIKAKATI MIZITO
Ndugu Mutafungwa Kamishina Msaidizi wa Barabarani amesema wamejipanga katika kuzibiti ajali barabarani kwa kuwachukulia hatua kali wale wote wasiofuata kanuni, Sheria na utaratibu wa sheria barabarani ndugu mtafungwa amepongeza shirika la afya duniani WHO kwakuisaidia serikali ya Tanzania dhidi ya mapambano ya kudhibiti ajali za barabarani kwa kuja na mradi wa kutoa elimu kwa wanahabari jinsi ya kuandika maswala ya barabarani pamoja na kuwapa elimu wanasheria amesema haya kwenye semina iliyowahusisha wanahabari Jijini Dar es Salaam nayo wizara ya Afya wamesema ajali barabarani zikipungua nchini zitasaidia kupunguza vifo kwa wingi na gharama za kuwatibu waga wa ajali zitatumika kwenye maendeleo ya nchi nao WHO wamawataka wanahabari kupaza sauti zao na watumie karamu zao vizuri ili ajali zisitokee nchini Tanzania.
Penina ni mwanahabari kutoka gazeti la majira kwa niaba ya wanahabari wenzake ameipongeza serikali, jeshi la polisi pamoja na WHO kwa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo jinsi ya kuandika habari za barabarani.
Habari na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment