Friday, 1 July 2022

TUME YA KUZIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA YATANGAZA VITA

 







Kamishna Jenerali Gerald Musabila Kusaya wa tume ya kuzibiti na kupambana na dawa za kulevya


Amesema yeyote atakaye kamatwa akiuza, kusambaza, kusafirisha au kutumia dawa za kulevya watamkamata na kumfungulia mashtaka tangu tume ianzishwe ina miaka mitano imekamata kilo 16600 na mwaka jana imekamata kilo elfu nane (8000) za dawa za kulevya amewataka watu kutumia namba ya simu ya 119 tena bure kwaajili ya kuwafichua wauzaji wa dawa za kulevya, kamishna ameongezea kwa kusema wamezibiti uingizaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja vya ndege pamoja na bandari changamoto wanayokutana nayo baharini kuna bandari bubu Zipatazo mia tano (500) pia atakaye toa taarifa kutakuwa na usili mkubwa.

Maswala ya kuandika vipeperushi pamoja na kitabu kitakacho zinduliwa kwa maandishi ya nukta nundu kwaajili ya wasioona tume inavifanyia kazi nae kwa upande mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amewataka watu kutotumia madawa ya kulevya kwani yanapoteza nguvu kazi ya Taifa.

habari Picha na Ally Thabit

No comments:

Post a Comment