Diwani wa kata ya Temeke Omary amesema yeye anatekeleza irani ya chama cha mapinduzi kwa vitendo ambapo wananchi wapatao 65 waliopitiwa na mradi wa mwendo kasi watalipwa pesa zao ujenzi wa miundombinu ya barabara unaendelea vizuri huku kwenye sector ya Afya wanaendelea kutatua vifo vya mama na watoto wachanga kwa vitendo pia amesema sasa wanajenga masoko ya kisasa maeneo ya vetenali na kuboresha masoko mengineyo diwani Omary wa kata ya Temeke amesema mradi wa ujenzi wa uwanjwa wa mwembe yanga unaofadhiliwa NORDIC kwa kupitia DMDP ambako kutakuwa na viwanja vya mpira wa miguu maeneo ya kupaki magari visimba kwaajili ya mama NTILIE sehemu ya kumpumzika pia maswala ya ndondi, ambako mradi huu ulianza tarehe 10/07/2022 na utamalizika mwezi kumi na moja.ambako umefika asilimia 85% na unathamani ya kiasi cha Tsh milioni 998, diwani wa kata ya Temeke amesema wanapambana na ukatili wa kijinsia ndani ya kata yake huku akimpongeza mkurugenzi wa manispaa ya Temeke Mkuu wa wilaya ya Temeke, Mtendaji kata wa kata yake na viongozi wote ndani ya kata ya Temeke bila kumsahau Aziza. Ametoa wito kwa watanzania na wasio watanzania waendelee kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kama Diwani wa Temeke Omary anavyofanya kwani amekuza elimu kwa ujenzi wa Madarasa.
Habari na Ally Tabith
No comments:
Post a Comment