Friday, 18 November 2022

TAASISI YA HATUA GROUP YAJA KUWAKOMBOA MAMA WAJAWAZITO

Mkurugenzi Derick Mgaya wa taasisi ya hatua group imeamua kuja na program ya mazoezi kwa mama wajawazito, elimu ya lishe na maswala ya kisaikolojia lengo kunusuru na kuokoa vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua na kabla ya kujifungua ambapo program hii itaanza mwezi wa pili 2023 uzinduzi umefanyika kwenye hospitali ya Mbagala Zakhiem. Nae kwa upande wake mkurugenzi wa vifaa vya kujifungulia wa mama wajawazito RENATUS ameunga mkoni juhudi na jitihada zilizofanywa na taasisi ya hatua group nae mwakirishi wa mkuu wa wilaya amesema ni vyema mama wajawazito kuunga mkono mradi huu kwani itawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimalisha Afya zao na watoto waliopo tumboni.

Nae Dakatari wa ushauri wa program hii ndug. Michael amesema watahakikisha wanawafikia mama wote wajawazito.

Habari kamili

Ally Thabith

No comments:

Post a Comment