William Erio Mkurugenzi mkuu mtendaji ya tume ya ushindani ya biashara Tanzania (FCC) amesema, lengo la FCC ni kuwaonganisha wafanya biashara wakubwa, wadogo na wakati ili waweze kupata ujuzi wa kiteknolojia na kuwaunganisha na kituo cha uwekezaji pamoja na wapate mitaji ya kutosha.
William Erio amewataka wafanya biashara wa Tanzania watengeneze bidhaa zenye unbora ili waweze kuuza ndani ya nchi na nje ya nchi pia amesema wanawafikia watu wenye ulemavu kwakuwapa elimu ya utengenezaji bidhaa zenye ubora katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania huku wakitumia wataalam wa lugha za alama kwenye mikutano yao na makongamano yao yanapokuwa wakitoa elimu kwa watu wenye uziwi. FCC mikakati yao nikutokomeza bidhaa bandia nasasa wana ofisi jijini mwanza ambako inahudumia mikoa ya kanda ya ziwa pia wamefungua ofisi Jijini Arusha na wako mbioni kufungua ofisi maeneo mengineyo.
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa FCC William Erio ametoa wito kwa jamii waitumie FCC
Amesema haya kwenye maonyesho ya saba ya bidhaa za ndani zinazotengenezwa na viwanda vya Tanzania Jijini Dar es Salaam nae kwa upande wake mfanya biashara Amiri Hamza ameipongeza FCC kwa kudhibiti bidhaa bandia hivyo ametoa lai kwa FCC waendelee na kazi yao nzuri.
Habari picha na Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment