Tuesday, 9 February 2021

AIRTEL YAPASUA ANGA


Airtel yaboresha mtandao kwenda masafa ya Supa-4G. Yaja na ofa kabambe za internet

  1. Ukianza kutumia aini ya Airtel utapata intaneti mara mbili bure BURE kwa kipindi cha miezi sita (Airtel dabo Data)
  2. Airtel imepunguza bei ya Airtel Mi-Fi kwa kurudisha GB 40 bure ili wateja wafuahie mtandao wa Airtel supa 4G kwenye simu za 3G.
  3. Airtel inatoa 7GB bure kwa wateja wote ambao watabadili laini kutoka 3G kwenda laini 4G
Dar es Salaam tarehe 09/02/2021. kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kukamilisha maboresho makubwa kwenye mtandao wake wa 4G kwenda kwenye masafa ubora zaidi ya Airtel Supa 4G ili wateja wake waendelee kuperuzi kwa uharaka zaidi popote. Akizungumza jijini Dar es salaam leo wakati wa kutangaza maboresho ya masafa hayo ya Airtel supa 4G, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa kwasasa "wateja wa Airtel kupitia maboresho ya mtndao wa Airtel Suapa-4G watapata huduma bora zaidi ya ilivyokuwa awali, watafurahia kuperuzi mtandao kwa kasi zaidi ndani ya miji mikubwa zaidi ya 500 nchini Tanzania iliyofanyiwa maboresho haya ya kufurahia huduma za kidigitali kama video za mfumo wa HD.

Tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika maboresho ya mtazamo wetu ili kukamilisha ahadi yetu ya kutoa huduma bora ya intaneti (Data) pamoja na huduma za kupiga simu kimataifa kwaajili ya wateja wetu.

Huduma ya Airtel Supa 4G inapatikana kwenye masafa y a700MHz NA 2100 MHz, ambapo kasi yake inawezesha wateja wetu sasa KUPERUZI kwenye mtandao kwa kasi ya 40Mbps kasi hii inafanya huduma yetu kimtandao kufikia viwango vya kimataifa zaidi na kwafaidisha wateja wote.

Mkurugenzi huyu wa mawasiliano wa Airtel Tanzani ameongeza kuwa kufuatia kuambaa kwa mtandao huu wa supa 4G, Airtel tumefanya mawasiliano kuwa nafuu zaidi kwa wateja wetu ili kufaidi mtandao wa Supa - 4G. Airtel saas imezindua huduma tatu kwa wateja ambazo zinapatika kwa kasi zaidi ili kuperuzi kutpita supa 4G ambazo ni 

  • Wateja wote wa Aitel ambao wanatumia laini za 3G endapo watabadilisha laini zao za simu kwenda kwenye mfumo wa 4G watapata ofa ya 7GB ndani ya wiki mbili bure
  • Ipo ofa ya intaneti mara mbili (Dabo data) kwa wateja ambao wataanza kutumia smartphone zao kwa mara ya kwanza na mtandao wa Airtel kwa miezi 6
  • Airtel tumepunguza bei ya Airtel Mi-Fi sawa na Tsh 75,000 ikiwa na 40 G0GB bure sawa punguzo la shilingi 30,000. Mi-Fi hii pia itawezesha wateja asio na simu za smartphone za 4G kutumia Mi-fi na kufurahia kasi ya Airtel Supa 4G yenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya wateja 10 kwa mara moja
Nae Meneja wa huduma za intaneti wa Airtel Ezekiel Kahatano ilielezea kuwa "uzinduzi wa Mtandao wa Airtel 4G-supa pamoja na kuanzisha ofa za bei rahisi za Airtel Supa 4G ni sehemu ya mipango ya Airtel ya kuboresha huduma za mawasiliano na kukuza utumiaji wa kuperuzi mtandao wa Airtel kwa kasi ya Airtel supa 4G kwani inakuja na teknolojia ya kisasa inayolenga kupunguza gharama za huduma za mawasiliano.

Habari na Ally Thabiti



No comments:

Post a Comment