Mashimba ndaki waziri wa mifugo na uvuvi amesema kuanzia tarehe 17 mwezi 12, 2021 kuku watauzwa kwa kilo, pia ameitaka Bodi ya nyama kwasambalatisha mara moja watu wanaouza vifaranga vya kuku eneo la Tazara wawasambaratishe mara moja na kampuni zinazo walazimisha wateja kununua kuku au chakula cha kuku hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na wale ambao wanatotolesha vifaranga vya kuku kienyejienyeji na wanaojifanya mawakala chamtema kuni watakipata maana selikari haiwezi kuwacha uhuni huu ufanyike kwani sector ya kuku ni sector muhimu nchini Tanzania ndio maana Rais Magufuli anaipa kipaumbele ili iweze kuchangia pato la Taifa.
Waziri Mashimba Ndaki amewatoa hofu na mashaka wafugaji wa kuku kuwa changamoto ya kodi na bei elekezi yakuuza kuku amelibeba na kulifanyia kazi.
Mashimba Ndaki amempongeza kaimu msajili wa bodi ya nyama kwa ubunifu wake kwa kuwakutanisha wadau wa sekta ya mifugo kwaajili ya kupata Suruhisho ya changamoto wanazokutananazo wadau hawa kwaajili ya masilahi mapana ya Taifa. Amesema haya jijini Dar es Salaam alivyokutana na wadau Mbalimbali wa Sekta ya mifugo.
Habari picha na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment