Imani Sichalwe kaimu msajili wa bodi ya nyama ameweza kuwakutanisha wafugaji wa kuku na wadau wanao uza chakula cha kuku vifaranga vya kuku, watalaam wa mifugo, benki ya CRDB pamoja na waziri wa mifugo na uvuvi Mashimba Ndaki lengo kukuza na kuistawisha sector ya ufugaji kuku ambapo changamoto zifuatazo ziliweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi ikiwemo ukuaji wa bei na viranga vya kuku kutoka shilingi 1700 hadi 2300 ambapo hiki ni kilio kikubwa cha wafugaji kuku Dar es Salaam. Bei ya chakula cha kuku bei yao imekuwa kubwa swala la kuuza kuku kwa kilo wafugaji wa kuku wamewasilisha kwa waziri na kutafutiwa masoko na machinjio ya kuku.
Kaimu msajili wa bodi ya nyama amesema amehitisha kikao hiki ili kumsaidia Rais Magufuli katika hazima yake ya ujenzi wa viwanda na kukuza uchumi wa Tanzania ambapo wafugaji hao wa kuku watasaidia kwa kiwango kikubwa katika kukua uchumi wa Tanzania, amewatoa hofu wafugaji wakuku nchini Tanzania kuwa Bodi ya nyama imewawekea mazingira ya rahisi na rafiki ili waweze kujikwamua kiuchumi na milango ipo wazi kwa watakao hitaji mawazo, ushauri na wataalam, amesema vikao hivi vitakuwa vinafanyika mara kwa mara huku akiwataka wauza viranga vya kuku na chakula cha kuku pamoja na chanjo za kuku wasiwakandamize na kuwaonea kwakuwauzia viranga vya kuku visivyokuwa na ubora dawa pamoja na chakula wakifanya hivyo watauwa mitaji ya wafuagaji kuku amesema. Amemshukuru waziri wa mifugo na uvuvi Mashimba Ndaki pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ilala kwa kuwaweza kuwasiliza wafugaji kuku na kutatua kero na changamoto zinazowakabiri wafugaji kuku.
Habai picha na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment