Wizara ya Ardhi Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema inahakikisha inatatua kero ya migogoro ya Urasmishaji wa ardhi inayowakumba wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam inamalizika katika kipindi kifupi.
Hayo yamesemwa leo na Waziri huyo wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mkoani Dar es salaam Jerry Slaa ambaye aliitwa jijini humo na Kamati Tendaji ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Dar es Salaam.
Katika kikao hicho kilichohudhuliwa na wataalamu wa ardhi kutoka halamshauri za Mkoa huo,kwa lengo la kujadili namna ya kuondoa tatizo la kero za urasmishaji wa ardhi zinazofanywa na baadhi ya makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha kutoka kwa wananchi huku yakishindwa kutekeleza majukumu yake.
"Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Watendaji wake kushughukia kero ya Urasmishaji wa ardhi inayowakumba wananchi wa Mkoa huo,"amesema Slaa.
Amsema Serikali imepanga kupima na kutoa hati za ardhi milioni mbili na laki tano(2.5 milioni) kufikia 2025,hivyo lengo la serikali ni kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi,kwa mikoa yote ishirini na sita(mikoa 26) nchini na kuna makamishna wa ardhi wanaotoa hati ,hatua hiyo inayosaidia wananchi kupata hati zao bila usumbufu.
Waziri Slaa ametoa muda wa siku saba kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi kuhakikisha wanatatua kero hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam nakwamba baada ya hapo warejeshe majibu kwa viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dar es salaam.
"Maelekezo yangu ya utatuzi wa kero ya Urasmishaji ni kuwa ,Naibu katibu Mkuu na Watendaji wenzako mlete taarifa kwa viongozi wa chama,kama kuna tatizo la fedha niambie ili tuone tunapata wapi fedha ili muweze kukamilisha kazi hii" amesema Waziri Slaa.
Aidha Waziri Slaa amesisitiza kwamba hataki kuskia kero za urasmishaji wa ardhi zinaendelea kujitokeza katika uongozi wake ambapo amesisitiza makampuni yanayojihusisha na urasmishaji huo yanapaswa kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na yale yatakayoenda kinyume yachukuliwe hatua za kisheria .
Ameongeza kusema kwamba "Urasmishaji umekua tatizo kubwa katika simu kumi anazopigiwa na wananchi simu saba hadi nane zinahusu malalamiko ya urasmishaji wa ardhi.
"Nimekuja na timu yangu inayohusika na mambo ya ardhi napenda kuagiza kuhakikisha kero hizi zinashughulikiwa haraka sana".
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Abass Mtemvu katika kikao hicho cha kamati tendaji cha CCM amesema kwamba Mkoa wa Dar es salaam umekua na tatizo la urasmishaji kutokana na kazi hizo kupewa makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha za wananchi nakutokomea nazo bila kufanya kazi hiyo kwa wakati.
Amesema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa waliona kumwita mheshimiwa Waziri wa Ardhi kuzungumzia tatizo hilo.
Katika kikao hicho madiwani,wakuu wa wilaya na wataalamu wa ardha walifika tayari , kupokea maelekezo ili kuondoa tatizo hilo.