Thursday, 28 March 2024

ACT YAWAPIGANIA WATU WENYE ULEMAVU KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Naibu Katibu mkuu wa mawasiliano na habari Shangwe Hayo ameitaka tume ya Taifa ya uchaguzi kuweka mazingira wezeshi pamoja na miundo rafiki kwa watu wenye ulemavu wanapokwenda kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mfano kuwepo kwa maandishi nukta nundu ili watu wasiona waweze kupiga kura kwa uhuru pia ameitaka serikali kupeleka mara moja mswada wa sheria ya uchaguzi amesema haya jijini Dar es Salaam makao makuu ya chama cha ACT Wazarendo wiliya ya Kinondoni.

Habari na Ally Thabiti

KANISA LA WRM LAJA NA TAMASHA LA KIBABE


Nabii Suguye amesema tarehe 01/04/2024 kanisa la WRM litatimiza miaka kumi na saba (17) tangu kuanzishwa kwake hivyo tarehe 01/04/2024 kutakuwa na tamasha siku ya jumatatu eneo la matembele ya pili kivule wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es Salaam ambako mgeni rasmi atakuwa Jerry Siraa waziri wa Ardhi. Nabii Suguye amesema kanisa la WRM linavyotimizwa miaka kumi na saba imeweza kutoa vifaa tiba kwenye hospitali ya Kivule matembele ya pili, uwekaji vifusi kwenye barabara ya kivule, ujenzi wa madarasa shule ya msingi kivule na shule ya sekondari kivule, pia wametoa misaada kwenye mikoa ya Mtwara, Lindi, Bukoba na Morogoro na wameanzisha vituo vya Tv na Radio vinakuja hivi karibuni.

Nabii Suguye amewataka Watanzania na wasio Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha lao siku ya jumatatu tarehe 01/04/2024 huku wakisisitiza pia wanamipango ya kuwasaidia watu wenye ulemavu na kuweka wataaramu wa lugha za alama kwa wenyeulemavu kwa wenye uziwi.

Habari Picha na Victoria Stanslaus

Tuesday, 26 March 2024

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AZINDUA KAMPENI

 





Waziri wa mambo ya ndani Masauni Jumanne Masauni amesema wameamua kuzindua kampeni ya kusajili jumuiya zote nchini Tanzania lengo kukabiliana na utakatishaji wa fedha kwenye jumuiya, uuzaji wa silaa kupitia jumuiya, uuzaji wa binadamu na kuzibiti vitendo vya ugaidi waziri masauni amewataka watendaji wa kata viongozi wa wilaya na wakuu wa mikoa kushirikiana ili kuweza kuzisajili hizi jumuiya ambako kwa ngazi za kimataifa itasaidia kukuza na kuimalisha demokrasia naye kwa upande wake msajili wa jumuiya wa wizara mambo ya ndani amesema kampeni hi ya usajili wa jumuia utaanza Dar es Salaam mwanza, Arusha na Mbeya lengo kuu kuweza kuendelea kuimalisha usalama ndani ya nchi ametoa wito kwa wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali waje kuwekeza Tanzania. Amesema haya jijini Dar es Salaam ukumbi wa Mwl Nyerere kwenye uzinduzi wa kampeni wa kusajili jumuiya.


Habari kamili na Ally Thabiti 

Thursday, 21 March 2024

tgnp yatoa mafunzo kwa wanahabari kuelekea uchaguzi

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa TGNP mtandao LILIAN LIUNDI amewataka wanahabari pamoja wanahariri wa vyombo vya habari kuhamasisha wanawake kushiriki katika kugombea nafasi za uongozi huku akiwaambia waelimishe jamii waachane na mira na desturi potofu dhidi ya wanawake wanapotaka kugombea nafasi za uongonzi amesema haya wakati akifungua mafunzo ya wanahabari kuhusu kuhamasisha wanawake wajitokeze kwenye serikali za mtaa, ubunge na udiwani ili wapate nafasi za maamuzi ngazi za juu. Amesema haya Mabibo Dar es Salaam.

Habari Picha na Ally Thabith



Tuesday, 19 March 2024

 Wakala wa Misitu wawafikia watu wenye ulemavu

kamishina wa wakala wa misitu Tanzania (TFS) Prof. DOS-SANTONS amesema katika miradi yao na utoaji wa Elimu wanazingatia watu wenye ulemavu.

kwa Mwaka jana mabubu walitoa semina katika Mkoa wa njombe huku mkoani Ruvuma kwa wenye uziwi kuna mradi wa ufugaji wa nyuki ,biharamuro pamoja na geita wakala wa misitu wamewapa mafunzo na kuwapa mitaji ya kulina asali na ufugaji wa nyuki katika shamba la SAO HILI , watu wenye ulemavu wanafanya shughuli za uvunaji miti na upandaji Miti.

Kamisha wa  TFS amesema katika utoaji wa Elimu kwa jamii wanatumia lugha za ALama kwa viziwi lengo la kufanya hivi kuweka fulsa sawa kwa wote , Amesema haya kwenye semina ya wahalili na vyombo vya habari.

kasi ya makusanyo ya fedha imeongezeka kwa kiwango juu ukilinganisha na mwaka 2015,ambapo walikuwa wakikusanya Bilioni 74.

kwa sasa wanakusanya kiasi cha Bilioni 175.huku akiwataka watu watumie Asali ya Tabaora maana ina ubora mkubwa.

ili kuandoa maswala ya hewa ukaa nchini Tanzania mkoa wa katavi wilaya ya Tanganyika unamradi wa kuondoa hewa mkaa na mkoa wa manyara eneo la wanzabe.

kila halimashauri inatakiwa wapande miti Milioni Moja na Laki 5 na Ardhi inafunikwa na miti hekta milioni 48,sawa na Asilimia 54 huku hekta milioni 47 za misitu zipo vijijini ,kilimo huchangia uwalibifu wa misitu asilimia 73.

Kamishina amewataka wahalili na wandishi habari kuelimisha juu ya utunzaji wa Misitu huku akiahidi ushirikiano kutoka tfs .

akisisitiza matumizi ya tekinologia na katika kukalibia na ulibiffu wa kukata miti , sheria kali zitawekwa.

Naye makamo mwenyekiti wa jukwaa la wahalili , salim amewataka wanahabari na wahariri wa habari , kuimiza jamii katika upandaji miti huku akipongeza kwa kuazisha viwanda 6 kwa ajili ya kuzalisha asali.huku akisisitiza kuazisha kwa haraka sheria kuzuiya matumizi na uwingizaji wa chain so

Habari picha :ALLY THABITI




Tuesday, 12 March 2024

STEVE NYERERE ATAKA HATUA ZICHUKULIWE KWA WANAOMTUKANA RAIS


Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama ongea na mwanao Steve Nyerere ameitaka serikali kuwachukulia hatua wale wote wanaomtukana na kumbeza Mhe Rais kwani kuna sera, sheria kanuni na miongozo kwa watu wanaotukana kwani hii itakuwa fundisho na adabu kwa wengine.

mwenyekiti wa taasisi ya Mama ongea na mwanao amempongeza rais kwa kuongoza vyema watanzania zaidi ya milioni 61 na ndani ya mika yake 3 ya uongozi amezesha kukuwa afya, Barabara, usimamizi wa reri ya umeme SGR na kutekeleza kwa vitendo mradi wa bwwa la mwalimu nyerere na kukuza sekta ya elimu na kuzingatia watu wenye ulemavu ndio maana taasisi ya Mama ongea na mwanao wameamuwa kugawa viatu kwa wanafunzi wa aina zote mpaka sasa wametoaviatu mkoa wa Tabora Anang'i, Bagamoyo na mikoa ngingine zaidi ya pea mia tatu (300), huku Steve Nyerere amewataka wanasiasa na wanaharakati kufanya kazi zao kwa kufuata sheria za nchi, huku wakiendela kwenye mikoa 13 ambako kauli mbiu inasema "MTONYE MWENZIO MAMA TENA" amesema haya wakati akiongea na wanahabari jijini Dar es Salaam Serena Hotel.

Habari na Victoria Stanslaus.

Thursday, 7 March 2024

VIONGOZI WANAWAKE WA TAASISI ZA SERIKALI WAMPONGEZA MHE.RAIS WA JMT DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Mheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima  amemshukuru Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha wanawake na kuwepo na kizazi chenye usawa.

Akiendelea kuzungumza katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 07, 2024 Mheshimiwa Waziri Dkt.Doroth alisisitiza uongozi huo kuchukua vikundi vya kina mama ili wawe na umoja ambao utasaidia kujadili ajenda za usawa na uchumi pamoja na kujadili mafanikio na masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto na jukwaa.

 "Niwapongeze kwa kuanzisha umoja huu hivyo Wizara inaahidi kufanya kazi na na ninyi katika kuongelea  mafanikio ya uwekezaji uliofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia," alisema Mhe.Dkt Dorothy.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki kutoka Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bi.Doreen Anthony Sinare amesema Umoja wa Viongozi Wanawake wa Mashirika, Taasisi na Vyuo vya Serikali wametoa tuzo kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta Maendeleo katika na kukuza Uchumi wa Taifa na kiongozi mwanamke wa mfano.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo  Doreen alisema umoja huo una jumla ya viongozi 31, na lengo la Umoja hii ni kuwafikia wanawake viongozi kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata, Wilaya na Mkoa ili kupata fursa mbalimbali.

Kwa upande wa Balozi Amina Salum Ali amewaomba wanawake kuungana ili wapate fursa na umoja huo unawajibu wa kushuka chini na kujua matatizo ya Wanawake wa waliongazi ya chini.

Nae Mkuu wa Ukuzaji Biashara na masoko kutoka Benki ya Mwalimu Commercial Bank Letcia Ndongole amesema wiki ya maadhimisho ya mwanamke duniani wameweza kuwekeza ili kuwafikia wanawake ngazi ya chini katika kukuza uchumi ambako asilimia 32% wanawake wamepiga hatua kwa kuwapa elimu kwenye kuwekeza na kuwapa mikopo hii yote ni katika kumsapoti mwanamke.

*Wekeza kwa mwanamke kuarakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii 

Habari na Victoria Stanslaus


Wednesday, 6 March 2024

 RAIS, Dr SAMIA SULUHU HASSANI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI OFISI ZA CCM.

Poul mkonda kaibu mwenezi taifa ,ccm amasema katika kumuenzi na kumkumbuka hayati ALHAJI AL HASSAN MWINYI , aliyekuwa Rais wa Tanzania Awamu ya pili ,Dr samia ameamua kutenga siku moja kila mwezi kuzungumza na wananchio juu ya kelo mbalimbali za wananchi.

kero hizi zitasikilizwa kwenye ofisi za ccm lumumba, dodoma na zanzibar.

poul makonda ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fulsa hii na kujitokeza kwa wingi kutoa kero zao huku akitoa tahadhali na kuwaonya watumishi na watendaji na wa ccm na serekali walioshidwa kutoa kero za wananchi kuchukuiwa hatua kali .

Poul makonda amebainisha hayo wakati alipokutana na wanahabari katika ofisi ya ndogo  ccm iliyopo lumumba Dar es salaaam.

alikuwa anawasilisha taalifa ya ziara yake aliyofanya katika mikoa 23 tanzania bara , kero kuu ilikuwa ardhi na ukatili wa watoto , utekaji wa watu na viongozi kutokutatua kero za watu.


Habari Picha na Ally Thabiti

 BODI YA MICHEZO YA KUBAHTISHA TANZANIA YAKUZA UCHUMI KWA KASI KUBWA .

Mkurungezi mkuu mtendaji wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Bwana JAMES , amesema ameweza kusaidia katika kukuza uchumi wa Tanzania kwa ongozeko la makusanyo ya kodi kila mwaka , utoaji wa vibali kwenye michezo ya kubahatisha na utoaji wa leseni kwa makampuni ya michezo ya kubahatisha .

ambako kwa muwekezaji kutoka nje uwekeza Dolla laki 5 . na muwekezaji wa ndani anatoa Dolla laki 3 .pia mwaka uliopita wamekusanya Fedha bilioni 170.

na mwaka huu Bodi ya michezo ya kubahatisha inampango wa kukusanya fedha Bilioni 200 na mpaka sassa wameshakusanya fedha bilioni 108 ndani y miezi 6.

ndugu james sector hii inasaidia kwa kiasi kikubwa.kuajili vijana wa kitanzania zaidi ya vijana elfu 25 kuajilwa. na makampuni 91 yamepewa leseni . ukilinganisha na miaka ya nyuma 28  tu .kwenye upande wa sector ya michezo .

mkurungezi mkuu mtendaji ametoa wito kwa wahariri na wanahabari kuelimisha jamii iliiyondokane na dhana potofu juu ya michezo ya kubahatisha .

na wenyewe waandike habari zenye mlengo za kuhamasisha jamiii na watanzania juu ya mchezo wa kubahatisha kwani kuna fulsa nyingi.

amesema hayo katika mkutano na wandishi wa habari uliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Taifa cha utalii.

Habari na Ally Thabiti.

Tuesday, 5 March 2024

MERIDIAN NA TIGO PESA YAZINDUA PROMOSHENI MPYA YA CHOMOKA NA BAJAJI

Dar es Salaam 5 Machi 2024, Meridianbet, kampuni inayoongoza ya kubashiri, inafurahi kutangaza ushirikiano wa kipekee na Tigopesa, kampuni inayotoa huduma bora ya malipo kwa simu, kuanzisha promosheni ya kusisimua inayolenga kuwavutia mashabiki wa kubashiri kote Tanzania, kuanzia Machi 5 hadi Aprili 31,2024, promosheni hii inaahidi zwadi na burudani kwa washiriki.

Allan Rwebogora, Mwakilishi wa Meridianbet Tanzania alisema, "Tunafurahi kushirikiana na Tigopesa kuanzisha promosheni hii ya kusisimua kwa wateja wetu wapendwa, Sisi Meridianbet, tuna dhamira ya kutoa thamani na burudani bora kwa wateja wetu, na promosheni hii ushaidi wa auminifu wetu."

Kila siku, wateja wote wanaoweka pesa kwenye akaunti zao kubashiri kwa zaidi ya Shilingi 25,000 za Tanzania watapata spins za bure kwenye michezo ya kasino, zikiwapa fursa ya ziada ya kushinda kwa kiasi kikubwa wakati wanafurahia michezo yao pendwa ya kasino na kubashiri na kutakuwa na Jackpot ya Milioni 200 mzunguko 250. 

Zawadi za wiki: Washiriki wana nafasi ya kushinda zawadi za kuvutia za wiki, ikiwa ni pamoja na bonasi ya 10% inayowekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao za kubashiri. Zaidi ya hayo, washndi watatu wenye bahati watachaguliwa kila wiki kupokea simu mpya za kisasa ambayo ubashiri wa meridianbet unaweza kupiga *149*10# bashiri kila siku kwa nafasi ya kushinda zawadi za kusisimua zaidi au tembelea kwenye tovuti www.meridianbet.co.tz . Zawadi kuu: Kama kilele cha promosheni, Meridianbet na Tigo zinafuraha kutoa zawadi kuu ya kipekee: washindi wattu wenye bahati kila mmoja atapokea Bajaji mpya, njia ya usafiri ya mtindo na rahisi inayoahidi kuboresha safari yao kila siku.

Naye Fabian Felician, Meneja biashara wa kampuni ya Tigo, anawahimiza wateja wa Tigo Pesa kuchukua fursa hii kwa kuweka pesa kwenye akaunti zao za kubashiri kwa kupiga *150*01#, Chagua Malipo ya Bili, kisha chagua na Ingiza namba ya Biashara 444999, ikifuatiwa na kiasi. 

Washindi watachaguliwa kupitia droo za kila siku, droo kuu ya wiki itafanyika kila Ijumaa na tangazo litafanyw kupitia mitandao yetu ya kijamii, Meridianbet na Tigo Pesa zinaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake kupitia promosheni zenye kuvutia na zawadi nyingi. Promosheni hii itaitwa "CHOMOKA NA BAJAJI. ameyasema hayo jijini Dar es Salaam.

Habari na Victoria Stanslaus