Thursday 7 March 2024

VIONGOZI WANAWAKE WA TAASISI ZA SERIKALI WAMPONGEZA MHE.RAIS WA JMT DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Mheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima  amemshukuru Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha wanawake na kuwepo na kizazi chenye usawa.

Akiendelea kuzungumza katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 07, 2024 Mheshimiwa Waziri Dkt.Doroth alisisitiza uongozi huo kuchukua vikundi vya kina mama ili wawe na umoja ambao utasaidia kujadili ajenda za usawa na uchumi pamoja na kujadili mafanikio na masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto na jukwaa.

 "Niwapongeze kwa kuanzisha umoja huu hivyo Wizara inaahidi kufanya kazi na na ninyi katika kuongelea  mafanikio ya uwekezaji uliofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia," alisema Mhe.Dkt Dorothy.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki kutoka Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bi.Doreen Anthony Sinare amesema Umoja wa Viongozi Wanawake wa Mashirika, Taasisi na Vyuo vya Serikali wametoa tuzo kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta Maendeleo katika na kukuza Uchumi wa Taifa na kiongozi mwanamke wa mfano.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo  Doreen alisema umoja huo una jumla ya viongozi 31, na lengo la Umoja hii ni kuwafikia wanawake viongozi kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata, Wilaya na Mkoa ili kupata fursa mbalimbali.

Kwa upande wa Balozi Amina Salum Ali amewaomba wanawake kuungana ili wapate fursa na umoja huo unawajibu wa kushuka chini na kujua matatizo ya Wanawake wa waliongazi ya chini.

Nae Mkuu wa Ukuzaji Biashara na masoko kutoka Benki ya Mwalimu Commercial Bank Letcia Ndongole amesema wiki ya maadhimisho ya mwanamke duniani wameweza kuwekeza ili kuwafikia wanawake ngazi ya chini katika kukuza uchumi ambako asilimia 32% wanawake wamepiga hatua kwa kuwapa elimu kwenye kuwekeza na kuwapa mikopo hii yote ni katika kumsapoti mwanamke.

*Wekeza kwa mwanamke kuarakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii 

Habari na Victoria Stanslaus


No comments:

Post a Comment