Nabii Suguye amesema tarehe 01/04/2024 kanisa la WRM litatimiza miaka kumi na saba (17) tangu kuanzishwa kwake hivyo tarehe 01/04/2024 kutakuwa na tamasha siku ya jumatatu eneo la matembele ya pili kivule wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es Salaam ambako mgeni rasmi atakuwa Jerry Siraa waziri wa Ardhi. Nabii Suguye amesema kanisa la WRM linavyotimizwa miaka kumi na saba imeweza kutoa vifaa tiba kwenye hospitali ya Kivule matembele ya pili, uwekaji vifusi kwenye barabara ya kivule, ujenzi wa madarasa shule ya msingi kivule na shule ya sekondari kivule, pia wametoa misaada kwenye mikoa ya Mtwara, Lindi, Bukoba na Morogoro na wameanzisha vituo vya Tv na Radio vinakuja hivi karibuni.
Nabii Suguye amewataka Watanzania na wasio Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha lao siku ya jumatatu tarehe 01/04/2024 huku wakisisitiza pia wanamipango ya kuwasaidia watu wenye ulemavu na kuweka wataaramu wa lugha za alama kwa wenyeulemavu kwa wenye uziwi.
Habari Picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment