Friday, 18 June 2021

BETI AWATAKA WATU KUJITOKEZA SIKU YA BABA DUNIANI

 Kila ifikapo tarehe 16 ya mwezi 6 ni siku ya baba duniani ambako BETI amewataka watanzania kutambua na kuthamini michango ya kina baba  . Pia amesema watu wakitambua umuhimu wa baba maswala ya ukatili wa kijinsia yatatokomea.

Habari na Ally Thabiti

JANETI MAWINZA ATOA MAPENDEKEZO KABAMBE YA BAJETI

 Janeti Mawinza ameitaka Serikali kuzingatia bajeti yenye mlengo wa kijinsia ikiwemo ujenzi wa mabweni  kwaajili ya wanafunzi wa kike pia kuwepo na bajeti kwaajili ya waanga wakifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia .

Habari na Ally Thabiti

BODI YA MIKOPO YAJA NA MUHARUBAINI


 Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Badu Masudi amesema wameamuwa kushirikiana na Rita Lengo kufanya uhakiki wa vyeti vya wanafunzi watakao pata mikopo ya Elimu ya juu.

Kwani kuna udabganyifu mkubwa unaofanywa na waomba mikopo na kupelekea watu wenye sifa kukosa mikopo .

Habari picha na Ally Thabiti 

WATUNISHA MISURI WATANGAZA VITA


 Katibu wa Chama cha Watunisha Misuri amewataka Vijana wa Kitanzania kujitokeza kwa wingi katika kushiriki kutunisha Misuri kwani kuna fursa mbalimbali zinapatikana za kujikwamua kiuchumi.

Habari picha na Ally Thabiti

MAMBO MOTO TV YAWATOA MCHECHETO WAPINZANI WAO


 Mkurugenzi wa Mambo Moto Tv amesema wameanzisha Tv hii Lengo kuwapa akira Vijana wa Kitanzania kuwa kuonyesha Tamthiria zao ambako Mambo Moto Tv inapatikana kwenye kisimbuzi cha Zuku na Dstv.

Habari picha na Victoria Stanslaus 


CCM TEMEKE YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA SULUHU HASANI


 Katibu Mkuu wa CCM Wilaya ya Temeke amesema wanamuunga mkono Rais SAMIA SULUHU HASANI kwa utendaji wake nzuri wa kazi kwani anjali makundi ya aina yote pia ni msikivu.

CCM Wilaya ya Temeke wanamshukuru kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya mwendo kasi eneo la mbagala Dsm .

Amewataka watanzania nawasio watanzania wenye vyama na wasio na vyama na viongozi wa Dini zote waendelee kumuunga mkono na kutoa moyo Rais SAMIA SULUHU HASANI katika kuiongoza nchi ya tanzania .

Habari picha na Victoria Stanslaus

KCB BANK YAJA KIVINGINE


 Pasko Machango Mkuu wa Fedha wa KCB BANK amesema wameamuwa kushirikiana na VETA Lengo kuwapa ujuzi na maarifa Vijana wa Kitanzania ili waweze kujiajili ,kusajiliwa na kuwaajili watu wengine.

Ambako Vijana zaidi ya 118 wameweza kupata mafunzo VETA ya kuchomelea mageti,upishi,upambaji,ulimbende na fani zinginezo.

Pasko Machango amewataka watu kutumia KCB BANK kwenye matawi ya Arusha,morogoro,mwanza,Dsm na Zanzibar kwani huduma wanazozitoa ni rafiki na zenye ubora mkubwa .

Habari picha na Ally Thabiti

 

VETA YAWASHA MOTO

Mkuu wa VETA Dsm Joph Mwanda amewataka Vijana wa Kitanzania kujiunga na VETAchang'ombe Dsm ili wapate ujuzi kwani Lengo la VETA Kuwainua na kuwakomboa kiuchumi na kimaisha kwa kuwapa mafunzo na fundi stadi wa aina zote.

Ametoa wito kwa watanzania kuwacha mawazo potofu kuwa VETA ni kimbilio  la Vijana walio feria mashuleni kwani si kweli na badala yake wajitokeze kwa wingi kupata Elimu ya VETA .

Joph Mwanda amewataka watanzania na wasio watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho ya 45 yatakayo fanyika viwanja vya sabasaba kuanzia tarehe 28ya mwezi 6 mwaka 2021 mpaka tarehe 13 ya mwezi 7 mwaka 2021 wajionee ndani ya banda la VETA bunifu mbalimbali 

Habari picha na Victoria Stanslaus 
 

REA KOMBA ASIKILIZA KILIO KIZITO CHA WADAU WA ELIMU


 Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Rea Komba amesema wameamuwa kufanya kongamano la wadau wa Elimu . Lengo kukusanya Maoni na mapendekezo ya mabadiliko ya mitahara kuanzia Elimu ya ngazi ya awari,msingi na secondary .

Amesema hiki kilikuwa Kilio cha muda mrefu cha wadau wa Elimu kuwepo kwa maboresho ya mitahara yetu nchini tanzania .

Rea Komba amesema mabadiliko haya yatazingatia kufikiwa kwa makundi yote wakiwemo watu wenye Ulemavu,wakulima ili nawao washiliki kikamilifu kwenye mabadiliko haya 

Habari picha na Victoria Stanslaus

TONY ROBGERS KABETHA AFUNGUA MIRANGO


 Mkurugenzi wa Universities Abrad ripresetative Tony Robgers Kabetha  amewataka wazazi na walezi kuchangamkia  furusa za kuwapeleka watoto wao kwenda kusoma nje ya nchi kwa gharama nafuu . 

Amesema wanapatikana Arusha ,mwanza eneo la barabara ya Kenyata ,Mbeya eneo la uindini na Makao Makuu Dsm  benjamin mkapa Tamwa gorofa ya pili . 

Pia ameipongeza taasisi ya Elimu kuja na mabadiliko ya mitahara yetu kwani itakuwa imeleta ukombozi na Mapinduzi makubwa katika Elimu ya tanzania .

Habari picha na Ally Thabiti

HENRY KULAYA AWA NA MATUMAINI MAZITO


 Mdau wa Elimu Henry Kulaya amesema mabadiliko ya mitahara yanayofanywa na taasisi ya Elimu endapo watazingatia kuwaongezea ujuzi na maarifa watawasaidia kwa kiasi kikubwa Vijana wa Kitanzania kuweza kujiajili,kusajiliwa na kuwaajili watu wengine .

Ameitaka Taasisi ya Elimu kwenye mabadiliko ya mitahara waboreshe maswala ya wanafunzi wenye maitaji maalum . Wakiwemo wenye uziwi,wasio Ona ,wenye ualbino,kuwepo kwa vifaa vyao na kuwepo na maandishi ya nukta nundu.

Pia mazingira ya walimu yakufundishia yaboreshwe na kuwepo na miundombinu rafiki kwa wanafunzi.

Habari picha na Victoria Stanslaus 

DR MGENDI ATOA NENO

Dr Mgendi ameitaka Taasisi ya Elimu kutengeneza Mitahara itakayotoa majawabu kwa watoto wa Kitanzania baada ya kumaliza masomo waweze kujiajiri .

Pia ameitaka Wizara ya Elimu kuondoa viboko mashuleni 

Habari picha na Ally Thabiti 
 

Friday, 4 June 2021

ZANZIBAR MAMBO SHWARI


 Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la wafanya Biashara  Zanzibar Bakari Haji Bakari amewataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi Zanzibar kwaajili ya kuwekeza .

Pia amesema wanamausiano mazuri na tanzania bars 

Habari picha na Ally Thabiti

TATOA YALIA NA MIRORONGO YA KODI


 Serikali ni vyema kupunguza mirorongo ya kodi kwa wafanya Biashara kwani imekuwa ni kikwazo  na inawaletea ugumu watu kuanzisha Biashara.

Pia kuna mkwamo wa kupunguza kodi ni vyema serikali iondoe mkwamo huu.pia kampuni ziwezwe kulindwa katika maswala ya kodi .

Habari picha na Ally Thabiti 

JOSEFU ATAKA KITENGO CHA MAPINGAMIZI


 Josefu ameitaka Serikali wawe na utaratibu wa kusikiliza mapingamizi ya walipa kodi .pia Mifumo ya sheria ya kodi kabla aijaanza kutungwa wawashirikishe wafanyabiashara.

Habari picha na Victoria Stanslaus 

Thursday, 3 June 2021

BRELA YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA


 Godfrey Nyaisa Afisa  Mtendaji Mkuu BRELA amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika kuandikisha kampuni zao kwani Mifumo yao ni raisi ambako amna maswala ya urasimu.

Pia BRELA inajivunia mafanikio makubwa .kwani kupitia Mifumo yao ya kieletroniki imeweza kuwafikia watu wengi kwa haraka .

Huku kunawapunguzia gharama za kusafiri kupelekea kwenye Ofisi za BRELA kwaajili ya kupata huduma mbalimbali na wameweza kuokoa muda kwa wateja wao kwa kujiajili wakiwa popote.  

Pia Mifumo yao ni Imara,madhubuti,makini na ina Usalama mkubwa.

Habari picha na Ally Thabiti

KAIMU MKURUGENZI WA IDARA YA VIWANDA ZANZIBAR ATOA NENO KWA SIDO


Khamisi Ramadhani kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda Zanzibar amewataka SIDO wawajengee uelewa na Uwezo wajasilimali wa Zanzibar namna ya kutengeneza Vifungashio kwenye bidhaa zao  na wawatafutie Masoko ya kutosha.

Pia waweze kupunguza gharama wanazotozwa kwaajili ya kutengeneza bidhaa .ametoa wito kwa wazanzibar kuwa wajasilia mali kwani watanufaika kwa mikopo isiyokuwa na riba.

Habari picha na Victoria Stanslaus   

DR CHARESI KASANZU AFUNGUA MILANGO KWA WACHIMBAJI WADOGO

 

Charesi Kasanzu amesema anawakaribisha wachimbaji wadogo ambao wanaoitaji kuwekeza kwenye sekta ya Madini .

Kwani wao gharama zao ni nafuu katika kufanya tafiti za maeneo ya uchimbaji Madini kwa gharama nafuu .pia wanatoa ushauri na Elimu  .

Mafanikio makubwa waliyoyapata wamegundua gesi na Madini amesema haya wiki ya utafiti na ubunifu Chuo Kikuu cha Mlimani.

Habari picha na Ally Thabiti

FLORA STEPHANO AJA NA MUHAROBAINI WA UGONJWA WA KUTETEMEKA


 Muhadhiri Idara ya Zuolojia na Uhifadhi Viumbe poli amesema wamefanya tafiti kwaajili ya kupata tiba ya ugonjwa  wa Kutetemeka

Ivyo utafiti huu utakuja kutatua maradhi ya Kutetemeka na kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Kutetemeka .Flora Stephano Ameipongeza serikali na wadau wengine kwa kutoa mchango wao kwenye mambo ya tafiti na bunifu. 

Habari picha na Ally Thabiti 

AMOSI MAKALA AJA NA MAAGIZO MAZITO


 Mkuu wa Mkoa wa Dsm Amosi Makala ameitaka jiji la Ilala kuwawekea utaratibu nzuri wamachinga kwani kwa sasa vibanda walivyojenga vinaatalisha Usalama wao na Wananchi.

Pia ameaidi kupita kata kwa kata ili kutatua kelo za Wananchi amepojea vilio vya Madiwani wa jiji la Ilala ivyo amesema kelo zote atazifanyia kazi ikiwemo ujenzi wa barabara,zahati ,hospitali.

Swala la Talura atazifanyia kazi Lengo kuondoa mnyukano uliopo na machinjio ya vingunguti yaweze kumaliziwa haraka .

Habari picha na Victoria Stanslaus

Wednesday, 2 June 2021

TRA YAKUTANA NA TCCIA

 Julias Mjenga Afsa Mkuu wa Huduma na Mtoa Elimu kwa Mlipa kodi TRA amesema wamekutana na wafanyabiashara Lengo kupokea changamoto wanazokutana nazo katika Biashara zao.

Hivyo amesema watazifanyia kazi na kuzitilea ufafanuzi kelo zote pia amesema wameandaa vitabu vya Nukta Nundu kwaajili ya wasiio Ona Lengo wawe na uwelewa na Elimu ya ulipaji kodi.

Habari picha na Ally Thabiti


 

NAIBU MEHA WA ILALA APAZA SAUTI


 Sadi Kimji Naibu Meha wa Ilala amewataka Talura kutoa ushirikiano na Madiwani wa Ilala na tanzania kwa ujumla kwani wamekuwa kelo nawasumbufu kwa Madiwani na watanzania . 

Mfano katika ukusanyaji tozo za kuegesha magari ,faini uegeshaji mbaya wa magari .

pia Talura wanajenga Vivuko,Madaraja ,barabara pamoja na Mitaro.ambako utakuta kunakuwaga na mapungufu makubwa na kukosekana kuimarika kwa muda mrefu miundombinu hii .

Hivyo ili kuondokana na mnyukano huu ni vyema Talura kuwa wasikivu na waelewa .

Habari picha na Ally Thabiti   

ACP MAHANGA ATOA NENO ZITO


 Mkurugenzi wa Michezo Jeshi la Polisi Tanzania ACP Jonas Mahanga amesema Jeshi la Polisi linawapongeza silent Ocean kwa kuweza kuwapa vifaa vya michezo lindo hiki kinafanya michezo uendelee na iimalike kwa Jeshi la Polisi.

Habari picha na Ally Thabiti

JESHI LA POLISI KINONDONI LAWATOA LAO NYA WATU


 ACP Ramadhani.H. Kingai Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni  amewataka wanakinondoni kupuuza taarifa za mitandaoni kwani Kinondoni kupo shwari kiusalama na Jeshi lake limejipanga kwaajili ya kukabiliana na vitendo vyovyote vya kialifu.

Mpaka sasa Jeshi la Polisi Kinondoni limedhibiti wizi wa magari na vifaa vya magari pamoja  na kuvunja nyumba za watu .

Kamanda wa Polisi Kinondoni Ramadhani . H. Kingai ametoa rai kwa wanakinondoni wakifanyiwa vitendo vyovyote vya kialifu waende kutoa taarifa Polisi nasio kukimbilia mitandaoni ili kuondoa hofu kwa watu amesema haya ostabei Polisi Kinondoni wakati akiongea na Wanahabari.

Habari picha na Victoria Stanslaus