Thursday, 31 March 2022

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII YAMPONGEZA RAISI SAMIA SULUHU HASSAN


Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia watoto na makundi maalum Dr. Doris Ngwajima amesema kipindi cha uongozi wa Raisi Samia Suluh Hassan kwa Mwaka Mmoja ameweza kuanzisha wizara ya maendeleo ya jamii ambako imeweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kutatua changamoto zilizo kuwa zinawakabili watoto waishio mitaani, wanawake na watoto pia pamoja na makundi maalum yameweza kufikiwa kwa kiasi kikubwa Waziri Doris Gwajima amewataka watu kumuunga mkono Rais Samia Suluh Hassan 




Nae katibu mkuu Dr. Zainabu Chaula amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kuyainua makundi mbalimbali hivyo ni vyema watu waendelee kumuunga mkono na kuwanao sambamba.

Habari picha na Ally Thabith

KAMPUNI YA PUMA YA MAFUTA YATOA ZAWADI

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Puma Energy Dr. Suleiman Madige lengo la kutoa zawadi nikuongeza ufanisi kwa Ma_meneja na wadau wa kampuni ya Puma. Ameutaka uongozi wa kampuni hii ifikapo mwaka 2025 Puma iwe na vituo vitavyo 150 ambavyo kwasasa vipo vituo 80 

Naye kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Puma amemuhakikishia mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya PUMA kuwa ifikapo mwaka 2025 watahakikisha watajenga vituo zaidi ya 150 pia mkurugenzi amepongeza serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan namna inavyoweka nguvu kwenye kampuni ya PUMA. Kwa upande wake VANESA meneja wa kampuni ya PUMA energy ametoa wito wa watu wote waendelee kutumia bidhaa ya kampuni ya PUMA pia kampuni ya PUMA inakuja na bidhaa ya gesi ambako gesi hiyo itapatikana kwenye vitu vyote vya PUMA, VANESSA amewaahidi watu waishio vijijini watajengewa vituo vya PUMA.

Habari  na Ally Thabith

 

Friday, 4 March 2022

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AWAFUNDA VIONGOZI WA DINI


 Hamadi Suleimani Chande  Naibu Waziri wa Fedha na Mpango amewataka viongozi WA dini Kutoa elimu Kwa jamii ,pia Watumie nafasi zao vizuri na waache kujikweza .

Habari picha na Ally Thabiti

WAZIRI APONGEZA KONGAMANO LA AFRICA MEDIA

 Waziri wa Ardhi Anjerina Mabura ameipongeza Kampuni ya Africa Media Group Kwa kufanya kongamano la Wanawake ambako umesaidia kutolewa Kwa madam mbalimbali za kuwawezesha Wanawake kuwainua kiuchumi na kutiwa moyo.

Habari na Ally Thabiti

TAASISI YA SAFINA YABAINISHA MIKAKATI


 Mkurugenzi wa Taasisi ya Safina amesema watashirikiana na serikali katika kuwajengea mazingira wezeshi watoto waishio mitaani Kwa kuwaweka pamoja na kuwapa ujuzi mbalimbali .

Mkurugenzi wa Safina amesema Taasisi yao wanawapokeana kuwapa Mafunzo watoto wa mitaani wenye Ulemavu wa Aina mbalimbali.

Habari picha na Ally Thabiti

SOS YAUNGA MKONO JUHUDI ZA DORITH NGWAJIMA


 Mkurugenzi wa SOS David amesema wanamuunga mkono juhudi na jitihada za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee,Watoto, Wanawake na Makundi Maalum katika kuwatengenezea mazingira wezeshi watoto waishio mitaani kwani vipaji vyao vitaonekana na wataweza kujikwamuwa kiuchumi.

Habari picha na Ally Thabiti

JAMES YUSTA AMEPATA TUMAINI KWA WAZIRI DORITH NGWAJIMA


 James Yusta amemshukuru na kumpongeza Waziri Dorith Ngwajima na viongozi wote wa wizarani Kwa kuja na Mpango Mkakati kwaajili ya kunusulu Maisha ya watoto waishio mitaani, pia James amemshukuru rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuguswa na kuwa na uluma na watoto waishio mitaani.

Habari picha na Ally Thabiti

WAZIRI NGWAJIMA AKUTANA NA WATOTO WANAOFANYA KAZI MTAANI


 Waziri wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Watoto na Wazee amesema Lengo la kukutana na Watoto wanaokaa mtaani na kufanya kazi kwaajili ya kuwatengenezea mazingira Rafiki na  wezeshi ili waondokane na hadha zilizopo.

Habari picha na Ally Thabiti

JUKWAA LA WAHARIRI LATOA PONGEZI KWÀ LHRC


 Mwenyekiti wa JUKWAA la Wahariri Ndugu Barile amesema Kwa niaba ya Wahariri wa Tanzania wanawapongeza na kuwashukuru LHRC Kwa juhudi na jitihada wanazofanya na kuleta mabadiliko ya sheria na Sera mbalimbali za Tanzania na kupigania haki za binadam.

Mwenekiti wa Jukwaa la Wahariri amesisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na LHRC.

Habari picha na Ally Thabiti

LHRC YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI


 Afsa Plogram Wakiri Msomi Maduhu amesema Lengo la LHRC kukutana na wahariri wa Vyombo vya habari ni kuweza kuishukuru na kuipongeza serikali ya Tanzania Kwa kupitia sheria namba 7 ya mwaka 2021 ya makosa ya jinai na maboresho ya sheria namba 2 inayouau maswala ya utakatishaji wa pesa .

Maduhu amesema serikali ya Tanzania imekuwa sikivu kwani imepokea maoni na mapendekezo ya LHRC kwaajili ya maboresho ya sheria,kanuni na vifungu mbalimbali vya sheria , Maduhu Amewapongeza wahariri wa Vyombo vya habari .

Nae Kwa upande wake Afsa wa LHRC Raimondi Kanegere amesema LHRC inaendelea kufanya kazi na serikali kwaajili ya kuwepo Kwa ufanisi mzuri nchini Tanzania ,Raimondi Kanegere ametoa wito Kwa serikali kuwashirikisha wadau mbalimbali pindi wanapotoa miswaada mbalimbali kabla ya kuwa sheria tena watoe Kwa muda WA kutosha  na wayafanyie KAZI  mapendekezo ya sheria.

Habari picha na Ally Thabiti

MKURUGENZI WA TRC AHAIDI KUTEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MAKAME MBARAWA

 Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema ifikapo mwezi wa 4 mwaka 2022 shirika la Reli (TRC) wataanza majalibio ya Trenni ya  Umeme ya Mwendo Kasi (SGR) Kwa kilometa 300 Dsm mpaka Morogoro .

Mkurugenzi Masanja Kadogosa amesema mradi wa SGR umekamilika Kwa asilimia 95 Maeneo yaliobakia watamaliza Kwa wakati ikiwemo Vituo vya SGR Karakana na sehemu yza kupoozea Umeme.

Habari na Ally Thabiti

WAZIRI MAKAME MBARAWA AIPONGEZA TRC

 Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amelipongeza Shirika la Reli (TRC) Kwa kusimamia na kutekelezwa Kwa vitendo na Kwa kuzingatia Uweredi Zaid Ujenzi wa Treni ya Umeme (SGR) ambako Kwa sasa kilometa 300 Kutoka Dsm kwenda Morogoro zimekamilika Kwa asilimia 95.

Waziri Prof Makame Mbarawa amesema SGR itasaidia Kwa kiasi kikubwa watu kupata Huduma Bora Kwa haraka na wakati,ambako kutasaidia kukuwa Kwa biashara ,kuongezeka Kwa Ajira ,watu kusafiri Kwa wakati na itasaidia kukuwa Kwa sekta mbalimbali. 

Mfano sekta ya kilomo Waziri Mbarawa amesema Lengo la serikali kuboresha Viwanja vya Ndege,Bandari na miundombinu mingineyo,Waziri Prof Mbarawa amewatoa moyo TRC kuwa serikali IPO nao bega Kwa bega.

Habari na Ally Thabiti

Tuesday, 1 March 2022

TAASISI YA KUPAMBANA NA UKIMWI YAJA KIVINGINE


 Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Maboko amesema wameamuwa kuja na mfuko wa kuchangia Fedha kwaajili ya Kupambana na kudhibiti Ukimwi . 

Habari picha na Ally Thabiti

MSHAURI MWANDAMIZI WA FACFTA AHAIDI MAZITO

Halima Mshauri Mwandamizi wa FACFTA amewahaidi watanzania mkataba walioingia wafanyabiashara wa Tanzania watapata Masoko mengi Ivyo mambo mazuri yatakuja zaidi.


Habari picha na Ally Thabiti

KATIBU MKUU WA BARAZA LA ULAMAA APONGEZA SEMINA


 Hassan Chizenga Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislam Ulamaa  amesema Aya Mafunzo yatasaidia Kwa kiasi kikubwa WAISLAM na wasio WAISLAM wataweza kutunza na kulinda Amani ya Tanzania na duniani Kwa ujumla .

Pia wataweza kukuza vipato vyao na uchumi wao ametoa wito watu kupenda kusoma vitabu vya dini.

Habari picha na Ally Thabiti

MKURUGENZI WA BONDE LA MTO WAMI AJA NA MIKAKATI MIZITO


 Mkurugenzi Mwandisi Eribariki Mmasi wa Bonde la Mto Wami amesema Wamezinduwa Mpango Mkakati wa kutunza na kulinda Bonde la Mto Wami ambako yatatolewa Mafunzo ya Aina mbalimbalikwa wakazi wanaozunguka Bonde la Mto Wami.

Pia vitaundwa vikundi vya Aina mbalimbali wakiwemo watu wenye Ulemavu kwaajili ya kuweza kujikwamuwa kiuchumi kupitia Bonde la Mto Wami.

Habari picha na Ally Thabiti

RAMADHANI PAZI WA JUMUHIYA YA WANAZUONI WA KIISLAM AIPONGEZA SAUDIA


 Mjumbe wa Jumuhiya ya Wanazuoni wa KIISLAM Tanzania Ramadhani Abdalla Pazi amewapongeza Wasaudia kwa kuwapa semina ya siku tatu kwani utawasaidia Kwa kiasi kikubwa katika kujikwamuwa kiuchumi , ametoa wito Kwa washiliki wote  Mafunzo walioyapata wayazingatie na wakawafundishe wengine .

Pia ameipongeza mwenyekiti Ramadhani Abdalla Ndauga Kwa kuratibu Mafunzo haya.

Habari picha na Ally Thabiti

WASAUDIA WATOA SEMINA KWA WAISLAM


 Kiongozi Kutoka Saudia amesema Wameamuwa Kutoa semina Kwa jumuhiya ya Wanazuoni Lengo kuwajengea Uwelewa na ufaam waaswala ya Uislam na Maendeleo , Katika maswala ya maandishi ya nukta nundu kwaajili ya wasio Ona watafanyia kazi .

Habari picha na Ally Thabiti