Thursday, 31 March 2022

KAMPUNI YA PUMA YA MAFUTA YATOA ZAWADI

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Puma Energy Dr. Suleiman Madige lengo la kutoa zawadi nikuongeza ufanisi kwa Ma_meneja na wadau wa kampuni ya Puma. Ameutaka uongozi wa kampuni hii ifikapo mwaka 2025 Puma iwe na vituo vitavyo 150 ambavyo kwasasa vipo vituo 80 

Naye kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Puma amemuhakikishia mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya PUMA kuwa ifikapo mwaka 2025 watahakikisha watajenga vituo zaidi ya 150 pia mkurugenzi amepongeza serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan namna inavyoweka nguvu kwenye kampuni ya PUMA. Kwa upande wake VANESA meneja wa kampuni ya PUMA energy ametoa wito wa watu wote waendelee kutumia bidhaa ya kampuni ya PUMA pia kampuni ya PUMA inakuja na bidhaa ya gesi ambako gesi hiyo itapatikana kwenye vitu vyote vya PUMA, VANESSA amewaahidi watu waishio vijijini watajengewa vituo vya PUMA.

Habari  na Ally Thabith

 

No comments:

Post a Comment