Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam Godwin Gondwe ameitaka jamii kuwathamini watu wenye mahitaji Maalumu ikiwemo Walemavu kwani wanapaswa kupatiwa haki kama watu wengine.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe (mwenye Miwani) akiangalia ubunifu wa kazi za sanaa zilizofanywa na Watoto wenye Mahitaji Maalum. |
DC Gondwe ametoa rai hiyo wakati wa tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalumu lililoandaliwa na Kijiji Cha Makumbusho ya Taifa lenye ujumbe usemao"Haki Sawa Kwa Wote" lengo ni kuwakutanisha Watoto wenye mahitaji mabalimbali ikiwemo ulemavu wa viungo na walemavu wa ngozi( Albino).
Aidha amesema kwamba Watoto wenye mahitaji maalum wanatakiwa,kutambuliwa, kuthaminiwa na kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu ili kuwafanya waweze kuishi katika maisha bora ,huku akikemea jamii kuacha vitendo vya unyanyapaa kwa Watoto hao.
" Nakipongeza Kijiji Cha Makumbusho ya Taifa kwa kuandaa tamasha hili ambalo limelenga kutambua thamani ya Watoto wenye ulemavu,natoa wito kwa jamii,taasisi na mashirika mbalimbali kuendelea kuwathamini watu wenye ulemavu" amesema DC Gondwe.
Watoto wenye ulemavu kutoka shule mbalimbali za msingi ikiwemo shule ya Mgabe,Shule ya Msingi mchanganyiko,Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu ,wamekutana kwenye tamasha hilo nakuweza kushiriki Mambo mbalimbali ikiwemo michezo na burudani.
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Kijiji Cha Makumbusho Bi.Wilhelmina Joseph amesema kwamba Makumbusho ya Taifa itaendelea kuthamini makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo Watoto wenye mahitaji mbalimbali ili kuwafanya wapate haki zao za msingi.
Watoto wenye Mahitaji Maalum wakionyesha burudani kwenye Tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalum lililoandaliwa na Makumbusho ya taifa Mkoani Dar es salaam. |
"Tumeandaa tamasha hili ili kuthamini haki za Watoto hawa ,hivyo sisi Kama Makumbusho ya Taifa tumeandaa tamasha hili la Watoto wenye mahitaji Maalumu na tukaweka kauli mbiu ya Haki Sawa kwa Wote" ili kuifanya jamii itambue kuwa hata watu wenye ulemavu wana haki sawa na wengine hivyo wasiwafiche majumbani" amesema Bi Wilhelmina.
Akizungumza kwa niaba ya Walimu Wenzake kutoka shule hizo Bw.Emanuel Ibrahim kutoka shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ( Salvation Army) amesema kwamba ulemavu siyo kushindwa hivyo wameiomba Makumbusho ya Taifa kulifanya tamasha hilo kuwa endelevu.
Habari Picha na Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment