Latifa Mohamed Hamisi, Mkurugenzi mkuu wa TANTRADE amesema maonyesho ya ALBAINI NA SITA (46) ya Sabasaba yatakayofanyika tarehe 28/06/2022 yatakuwa yenye kufana na mafanikio makubwa ambapo nchi zaidi ya sabini (70) zitashiriki na kwa wafanya biashara watanzania wataonesha bidhaa zao amewataka watu kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya sabasaba kwani kiingilio ni nafuu na miundo mbinu yote imeboreshwa pia kutakuwa na makongamano ya aina mbalimbali lengo kuwatafuia fursa wafanyabiashara wa kitanzania na wageni kutoka nchi za nje kuwaonesha fursa za uwekezaji nchini Tanzania ambako kauli mbiu kwa mwaka huu inasema "Tanzania ni mahali sahihi kwa usalama wa biashara na uwekezaji". Bi. Latifa Amesema haya kwenye semina iliyowakutanisha wafanya biashara watakao shiriki kwenye maonesho ya sabasaba. Maada zilizowasilishwa ni Afya, ambaye aliwasisha Rehema kutoka halmashauri ya Temeke amesisitiza na UVICO 19 ambako chanjo zinapatikana za UVICO 19. Wa pili, Loyce Kibuta, Ameelezea namna ya kujikinga na majanga ya moto na jinsi yakutumia vifaa vya kuzimia moto nawataka watu kupiga namba 114 la jeshi la zima moto kwaajili ya msaada.
Abdallah Seif Abdallah amewataka wafanyabiashara kutoa risiti na wanunuaji wa bidhaa kudai risiti ambaye atatoa risiti atapigwa faini ya shinilingi milioni tatu mpaka milioni nne na nusu na atakae nunua kitu bila kudai risiti atatozwa elfu thelathini mpaka milioni moja na nusu.
Nora wa Tantrade amezungumzia tuzo za banda bora ambazo zitakuwa na category 26 nae SUDI afisa biashara wa Tantrade amezungumzia mfumo wa vibali.
Kwa upande wake Masha amezungumzia kanuni za ushiriki
Haya ndiyo ambayo yamezungumziwa kwenye semina kati ya Tantrade na washiriki wa maonyesho ya sabasaba.
habari Picha na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment