Maafisa wa usalama wa Pakistani walimkamata Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan siku ya Jumanne alipokuwa akifikishwa mahakamani katika mji mkuu, Islamabad, kujibu mashtaka ya kesi nyingi za ufisadi, maafisa wa chama chake walisema.
Khan alitolewa nje na kuwekwa ndani ya gari la polisi na maajenti kutoka taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo, Ofisi ya Kitaifa ya Uwajibikaji, kulingana na Fawad Chaudhry, afisa mkuu wa chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf.
Televisheni huru ya GEO ya Pakistan ilitangaza picha za Khan mwenye umri wa miaka 72 akivutwa na vikosi vya usalama kuelekea kwenye gari la kivita, ambalo lilimchukua.
Khan aliangushwa kwa kura ya kutokuwa na imani naye Aprili 2022. Amedai kuondolewa kwake kulikuwa kinyume cha sheria na njama ya Magharibi na amefanya kampeni dhidi ya serikali ya mrithi wake, Waziri Mkuu Shahbaz Sharif, akitaka uchaguzi wa mapema.
Chama cha Khan kililalamika mara moja kwa Mahakama Kuu ya Islamabad, ambayo iliomba ripoti ya polisi kuelezea mashtaka ya kukamatwa kwa Khan.
Maafisa wa shirika la kupambana na ufisadi walisema kuwa Ofisi ya Kitaifa ya Uwajibikaji ya Pakistan ilitoa hati za kukamatwa kwa Khan wiki iliyopita katika kesi tofauti ya ufisadi, ambayo hakupata dhamana jambo ambalo litamlinda dhidi ya kukamatwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Maafisa hao, ambao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina, walisema Khan atafikishwa mbele ya mahakama ya kupinga ufisadi baadaye Jumanne.
Hakukuwa na taarifa nyingine rasmi kutoka kwa serikali kuhusu kukamatwa kwa Khan.
Habari Picha na Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment