Wednesday, 31 January 2024

WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII NI TEGEMEO KATIKA SEKTA YA AFYA


Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Isdori Mpango kw niaba ya Mhe Dkt Rais Samia Hassan Suluhu. Makmu wa Rais amesema ifikapo mwaka 2030 madaktali na watoa huduma ya afya ngazi ya jamii itaboreshwa kuanzia miundombinu vituo vya afya, Zahanati Hospitali maalumu Hospitali ya kanda pamoja na rufaa.

Mpaka sasawashanunua magari 589 amburance vitanda 375, vifaa kwaajili ya uhangalizi wa watoto wachanga 125. Serikali imepanga kuajili na kuwejengea uwezo watoa huduma ngazi ya jamii 137294 ambao watachaguliwa ngazi ya vijiji usika kila sehemu kutakuwa na mwanamke na mwanaume kwenye vijiji vyote 68 ili kuondoa msongamano wa watu kwenye vituo vya kutolea huduma, katika mpango huu elimu ya Afya huduma mkoba, huduma kinga kabla ya kutoa rufaa kipaumbele kitakuwa lishe, afya ya Mama, maralia, Ukimwi kifua kikuu na mabadiliko ya tabia ya nchi.

zoezi la kuchaguliwa wahudumu wenye sifa stahiki kusiwepo na upendeleo wala rushwa, Bilioni 899.83 zimetengwa serikali imeandaa mpango jmuishi ili kuimarisha utoaji wa afya. Taratibu za mafunzo afya jumuishi za kinga kwa niaba ya Rais amewashukuru wadau wa maendeleo pia amesema mambo sita yafuatayo:-

1. Kuimiza mpango kufikia malengo

2. Taarifa za utekelezaji unafanyika

3. Kutumia mfumo wa kidigitali pia wanaweza kujifunza kwa wazanzibar ambao wameshaanza kutekeleza mradi huu.

4. Kutoa ushirikiano wa kutosha.

5. Wahudumu kuzingatia weredi na kujituma.

6. maswala ya lishe bora yasiachwe nyuma na kuzibiti magonjwa kama mararia na kipindupindu.

Haya ndio mambo sita muhimu ya kuzingatia kama serikali itawalinda na kushirikiana nao. wito amemtaka waziri wa afya kuanza mapema kuangalia wahudumu ngazi ya afya jamii ili ione serikali ina tambuwa mchango wao.






Habari Picha na Victoria Stanslaus

Friday, 26 January 2024

TAFA YAMPONGEZA KAMISHNA WA FORODHA

Makamo wa Rais wa TAFA Wahdi Saudin amesema utendaji wa FORODHA nchini Tanzania ni mzuri ambapo unawasaidia kwa kiasi kikubwa wafanya biashara kuingiza bidhaa zao na kusafilisha nje ya nchi bila matatizo makamo wa rais wa TAFA amemuomba kamishna wa FORODHA aweze kuimalisha mifumo ya FORODHA kwa njia ya kitekenolojia ili waendane na kasi ya dunia amesema haya siku ya FORODHA duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Habari na Ally Thabiti

KAMISHNA WA FORODHA AELEZA MIKAKATI MIZITO

Kamshina Forodha Juma Hassani amesema katika siku ya kuhazimisha siku ya Forodha leo hii wanajivunia watu wanavyotoa ushirikiano wa kulipa kodi bila shuruti na kupelekea biashara Tanzania kukua na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi kubwa. Pia wameweka mfumo wa single window huku wakizibiti ungizwaji wa bidhaa haramu na feki na kwa upande wake kamishna wa TRA Alufayo Kidata amesema forodha inawezesha kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa fedha nchini Tanzania nae kwa upande wake mkuu wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Kamanda Jumanne Mulilo amesema wataendelea kuzibiti na kulinda mianya wa ungizwaji na utoloshwaji mizigo kwa njia za panya huku wakiendelea kuimalisha ulinzi na usalama kwa wawekezaji nae kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilala akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Edward Mpogolo amesema wafanya biashara wasiwe na tabia za kuleta migomo watumie njia za malidhiano huku akiwataka watumishi wa TRA kuwa na maadili mazuri.

Habarai Picha na Ally Thabiti 

TIGO YAENDELEA KUIMALISHA HUDUMA ZAO


Emmanuel Mfanyakazi wa Tigo amesema licha ya changamoto ya mvua zinazoendelea nchini Tanzania na kualibu miundombinu ya mawasiliano mfano kunduchi kusombwa kwa daraja na bomba kuondolewa na maji na mkongo wa mawasiliano kuondolewa na maji tigo imefanya maboresho kwa kujenga miundombinu ya mawasiliano na kulejesha 5G na data huku wakitengeneza njia moja ya mawasiliano na kuweka njia mbadara.

Bw. Emmanuel amesema kiasi cha Tilioni moja cha fedha kimewekwa kwaajili ya uwekezaji ndani ya Tigo na mpaka sasa kiasi cha fedha cha nusu yake kimetumika kwa Dar es Salaam na Zanzibar imefika 80% ya 5G ambapo Network yake imekamilika huku mikoa ya Mwanza, Tanga, Morogoro na Mikoa mingineyo kiwango cha 5G ni 50% huku jitihada zikihimalika kuboresha 5G vijiviji vyote hapa nchini.

Tigo walipata tenda kutoka serikalini 30% kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya mawasiliano Ndg Emmanuel amesema haya wakati wa kukabidhiwa tuzo na kampuni ya Ookla.

Nae kwa upande wake Bw. John kutoka Tigo amesema tigo imejitahidi kutoa huma iliyobora na yakisasa na kupelekea uchumi wa Tanzania kukua na uchumi wa mtu mmoja mmoja kukua kwa kasi ambako imepelekea watu kupata taarifa kwa kitekenolojia mfano Taarifa za kilimo, Uvuvi, Biashara na Sekta zinginezo.

Bw. John amewapongeza wateja wa Tigo Milioni 16 kwa kutumia huduma zao.

Habari na Vitoria Stanslaus

Thursday, 25 January 2024

WAZIRI MCHENGERWA ATANGAZA VITA KALI

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewataka wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Tarura kujenga barabara zenye ubora pamoja na mifereji na makaravati wakishindwa kutekeleza miradi hiyo kwa ubora na kwa muda hatua kali zitachukuliwa juu ya mameneja wa Tarura na Wakandalasi huku akiwataka fedha wanazozikusanya wazitunze na wazitumie kwa uwalisia.

Habari na Ally Thabiti

KITABU CHA JAJI KISANGA CHAZINDULIWA

Tangu afeJaji Kisanga sasa ni miaka sita ndiyo maana Jaji mkuu wa Tanzania pamoja na familia ya Jaji Kisanga wameamua kuzindua kitabu ili jamii wajifunze mema aliyofanya kwenye upande wa sheria.

Habari na Ally Thabiti

CHADEMA YAMPONGEZA RAIS SAMIA

Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Bw. Mbowe amempongeza Rais DR. SAMIA SULUHU HASSAN kwa kukuza na kuimalisha demokrasia Tanzania amesema haya wakati wa maandamano.

Habari na Ally Thabiti

MERY NDARO AIMIZA WANAWAKE KUSHILIKI KWENYE CHAGUZI

Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake uwongozi na katiba Bi Mery Ndaro amewataka wanawake nchini Tanzania kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali huku akiitaka kamati ya Bunge, Sheria na Katiba kubadili sheria za uchaguzi ili wanawake, na watu wenye ulemavu waweze kushiriki kwenye uhaguzi nae kwa upandewake Mwenyekiti wa bodi ya TGNP Mama Gema Akilimali ameitaka serikali pamoja na Bunge kuzingatia usawa wa kijinsia katika chaguzi huku Bi Elen Kijo Bisimba akiimiza kupiga vita maswala ya rushwa ya ngono katika uchaguaji wa viti maalumu kwa wabunge na madiwani.

Habari na Ally Thabiti.

KAMANDA MULIRO AWATAKA CHADEMA WAENDELEE NA MAANDAMANO

Mkuu wa Jeshi la Polisi kanda maalumu ya mkoa wa Dar es Salaam Kamanda Jumanne Muliro amekipongeza Chama cha CHADEMA kwa kufanya maandamano ya amani na kuata utaratibu hivyo ametoa wito kwa vyama vingine vya siasa na CHADEMA yenyewe wakiendelea kufanya maandamano ya amani watapewa vibali bila matatizo.

Habari na Ally Thabiti

JANETH MAWINZA KUTOA ELIMU YA UWONGOZI

Mkurugenzi wa Wajiki Janeth Mawinza ameupongeza mtandao wa uwongozi kwa wanawake kwa kuweza kutoa tamko juu ya maswala ya ushiriki wanawake kwenye uchaguzi pia ametaka elimu itolewe kwa kiwango kikubwa ili wanawake waweze kugombea uwongozi.

Habari na Ally Thabiti

UFAULU WA WASICHANA WAZIDI KUPAA




Habari Picha na Ally Thabiti 

Thursday, 18 January 2024

TENMET YAFURAISHWA NA MABORESHO NA MITAALA MIPYA


 Bi Nasra wa TenMeT ameipongeza na kuishukuru serikali kupitia Taasisi za Elimu kwa kuboresha mitaara mipya kwani kaongeza ufaulu na vijana kuweza kujiajili na kuajiliwa pindi wanavyomaliza masomo ya serikali.

TenMeT kwa kushirikiana na wadau wao wa Elimu, watatoa elimu kwa jamii kuhusu maboresho ya mitaara ya Elimu

Habari Picha na Ally Thabiti

DKT. ANETH KOMBA AKUTANA NA WADAU WA ELIMU


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Aneth Komba emkutana na mtandao wa Elimu Tanzania leongo ni kuwaeleza maboresho ya mitaala mipya ya elimu ya mwaka 2023 ambapo kutakuwepo na mafunzo ya mali kwa mgazi ya Sekondari  ambako 99.7% kata za Tanzania zimepewa elimu ya maboresho ya mitaala mipya huku shule za sekondariza serikali zipatazo 28 zitato elimu ya hamali na shule 68 za Sekondari za watu Bonafsi nazo zitatoa mafunzo ya elimu ya hamali lengo nikuandaa vijana wa Tanzania wakimaliza elimu ya sekondari waweze kujiajili au kuajiliwa.

Dkt. Aneth Komba amesema elimu ya msingi itakuwa mwisho darasa la sita.

Habari picha na Ally Thabiti

Wednesday, 17 January 2024

TUMIENI FURSA YA MPAKA KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI NA KUIMARISHA UCHUMI _ DC ILEJE

 

Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mheshimiwa Farida Mgomi amewataka wananchi kushirikiana kikamilifu na vyombo vya usalama wilayani humo kwa kubaini wahalifu na uhalifu ili hatua zichukuliwe mapema.

Mheshimiwa Mgomi amesema hayo Januari 15, 2024 wakati akizungumza na watumishi wa kada mbalimbali wakiwepo uhamiaji, jeshi la polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania wilaya ya Ileje (TRA), afya, kilimo, na mifugo katika boda ya Isongole ambayo ni mpaka wa Tanzania ma Malawi huku akiwakumbusha majukumu yao ikiwepo kutoruhusu kuvushwa kwa magendo.

Mheshimiwa Mgomi amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kila mtu kusimamia majukumu yake kwa kusaidia mwingiliano huu ambao pia inasaidia kuimarisha uchumi.

Mheshimiwa Mgomi amesema mpaka huu wa boda ya Isongole wilayani hapa uwe chachu ya kuwasaidia wanaileje kunufaika kiuchumi kupitia ninyi wataalamu mliopewa dhamana ya kuhakikisha mnadhibiti viashiria vya magendo ambavyo vinasababisha kupiteza mapato ya serikali.

“Kila mtumishi kwa nafasi yake hapa mpakani awajibike ipasavyo na kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi waishio mpakani kutumia fursa ya mpaka huo kujiingizia kipato kwani asilimia kubwa wananchi wa Malawi wanatumia mpaka huo kufuata bidhaa Tanzania ikiwepo Isongole na Tunduma hivyo serikali kupata mapato na wafanyabiashara kujiongezea kipato. Ni jukumu letu kila mmoja tujipange vizuri kuhakikisha kwamba nchi zetu mbili zinabaki kuwa salama” amesema Mheshimiwa Mgomi.

Aidha DC Mgomi amesema kutokana na wilaya ya Ileje kupakana na nchi jirani ya Malawi, amewataka watumishi hao, kuimarisha usalama ,mahusiano ya ujirani mwema, kukusanya mapato ya serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara ili biashara zao ziweze kuwa na tija na hatimaye kusaidia ongezeko la mapato ya serikali.

Habari Picha na Ally Thabati 

MNYETI - MAAFISA MIFUGO NENDENI KWA WAFUGAJI, ACHENI KUWA WAKUSANYA MAPATO.

 


 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza baada ya kuzindua Baraza la Veterinari Tanzania awamu ya sita jijini Dodoma ambapo amewataka maafisa mifugo nchini kufanya kazi za udaktari wa mifugo walizosomea na kuwatembelea wafugaji badala ya kuwa wakusanya mapato wa halmashauri.



Katibu Mkuu Wizara ya Mifuo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amebainisha kuwa ana imani maafisa mifugo ambao walikuwa wakituma maombi kwa ajili ya kusajiliwa kwenye Baraza la Veterinari Tanzania sasa wataanza kusajiliwa rasmi kwa kuwa baraza hilo tayari limezinduliwa. Prof. Shemdoe amesema hayo wakati wa uzinduzi wa baraza hilo awamu ya sita.


Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania Prof. Lughano Kusiluka akizungumza wakati wa uzinduzi baraza hilo awamu ya sita jijini Dodoma ambapo amesema baraza limekuwa likisimamia sheria za veterinari kwa kuhakikisha wataalamu wanaohusika na kutoa huduma za afya za wanyama wafugwao na wasiofugwa wanafanya kazi kwa kufuata sheria na maadili.



Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt. Amani Kilemile akitoa neno la shukran pamoja na maelezo mafupi juu ya wajumbe wa baraza ambao wameteuliwa watakaodumu kwa miaka mitatu wakati wa uzinduzi baraza hilo awamu ya sita jijini Dodoma.



Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti akiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Riziki Shemdoe, Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania Prof. Lughano Kusiluka, Msajili wa baraza hilo Dkt. Amani Kilemile pamoja na wajumbe wa baraza hilo baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dodoma. (Picha na Edward Kondela – Afisa Habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

Na. Edward Kondela


Maafisa mifugo nchini wametakiwa kufanya kazi za udaktari wa mifugo walizosomea na kuwatembelea wafugaji badala ya kuwa wakusanya mapato wa halmashauri.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amebainisha hayo mjini Dodoma wakati akizindua Baraza la Veterinari Tanzania awamu ya sita baada ya baraza hilo kupata wajumbe.

Mhe. Mnyeti amesema baadhi ya maafisa mifugo wamekuwa wakijikita zaidi kwenye kukusanya mapato ya halmashauri minadani badala ya kuwatembelea wafugaji ili kujua matatizo yao.

“Maafisa mifugo kwenye halmashauri wanajifanya watumishi wa halmashauri kwa ajili ya kukusanya mapato kwenye minada kukusanya ushuru wa ng’ombe badala ya kufanya kazi za udaktari na kuwatembelea wafugaji.” Amesema Mhe. Mnyeti

Aidha, amelitaka Baraza la Veterinari Tanzania kuhakikisha linachukua hatua zaidi kwa maafisa mifugo ambao wamekuwa wakifanya kazi kinyume na maadili pamoja na kuwapatia semina mara kwa mara ili kuwakumbusha wajibu wao kwa wananchi.

Amesema pia ifike wakati maafisa mifugo ambao wanakiuka maadili wafukuzwe kazi pamoja na kufutiwa leseni zao ili kazi hiyo ifanywe na watu ambao watafuata taratibu na maadili ya kazi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifuo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amesema ana imani maafisa mifugo ambao walikuwa wakituma maombi kwa ajili ya kusajiliwa kwenye Baraza la Veterinari Tanzania sasa wataanza kusajiliwa rasmi kwa kuwa baraza hilo tayari limezinduliwa.

Amefafanua kuwa amekuwa akipata ujumbe kwa njia ya simu kutoka kwa baadhi ya maafisa mifugo ambao wamekuwa wakihitaji kusajiliwa lakini hawakuweza kusajiliwa kwa kuwa baraza halikuwa na wajumbe.


Naye Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania Prof. Lughano Kusiluka amesema baraza limekuwa likisimamia sheria za veterinari kwa kuhakikisha wataalamu wanaohusika na kutoa huduma za afya za wanyama wafugwao na wasiofugwa wanafanya kazi kwa kufuata sheria na maadili.

Ameongeza kuwa kazi kubwa ya baraza ni kuwaandikisha na kuwaingiza kwenye daftari la baraza hilo na kufuatilia kiwango na huduma wanazotoa, kusimamia elimu ya wanyama inayotolewa na taasisi mbalimbali na kufuatilia kwa ukaribu wadau wapate huduma inayotakiwa.


Baraza la Veterinari Tanzania awamu ya sita lililozinduliwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti litadumu kwa miaka mitatu.

Habari Picha na Ally Thabiti

CHADEMA YATOA MSIMAMO WA MAANDAMANO TAREHE 24/01/2024

Katibu Mkuu wa Chama cha Chadema John Mnyika amewataka watu kujitokeza kwa wingi tarehe 24/01/2024 kwa ajili ya maandamano ya siyokuwa na kikomo. John Mnyika amewataka watu kutoogopa jeshi la Polisi, Fidifosi na JWTZ kwani maandamano ya Chadema ni yaamani huku akisisitiza kuyapuuza maneno ya wanasiasa pamoja na wana CCM wanaopinga maandamano hayo.

Habari na Ally Thabiti
 

VYAMA KUMI NA TATU VYALAANI NA KUKEMEA MAANDAMANO YA CHADEMA

Mwenyekiti wa vyama kumi na tatu ambazo avina wawakilishi bungeni wanakitaka chama cha Chadema kusitisha maandamano yao ambao yatalajiwa kufanyika tarehe 24/01/2024 huku akiwataka wananchi kuto kushiki kwenye maandamano ya Chadema kwani watapata madhala makubwa mfano vifo, ulemavu wa kudumu, ualibifu wa miundo mbinu na athali za kiuchumi mwenyekiti Abdul Mluya ametoa wito kwa watanzania waendelee kumuunga mkono Raisi Dkt Samia Suluhu Hassani kwa uwongozi wake ulio mzuri ambao unazingatia maslahi ya Taifa na mtu mmoja mmoja huku akiishi na falsafa ya R4.

Habari na Ally Thabiti

Wednesday, 10 January 2024

MKURUGENZI MKUU WA BANDARI AINISHA MIKAKATI MIZITO

 




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mr. Plasduce M. Mbossa amesema wameanza kazi za kutanua Bandari ya Dar es Salaam kwa kujenga Magati kuanzia namba 12 hadi 15 magati haya yanauwezo wa kupakia Meri kubwa pia watajenga vituo viwili vya mafuta pamoja na kujenga Mapipa ya kupakulia mafuta Mr. Plasduce M. Mbossa amesema eneo la kulasini EPZA itakuwa bandari kavu kwa ajili ya kuweka Contena kwa wingi, pia kutakuwa na maboya ya kuongozea Meri uku wakiongeza kina kwenye magati.

Huku ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo unaanza hivi karibu ambako wataanza kujenga magati mawili ambako gati moja gharama yake Bilioni Moja Mia Tatu Siti kila gati litakuwa na ulefu wa Mt 500 ambako gati moja linauwezo wa kupokea meri moja yenye uwezo wa kubeba Makontena elfu 25 bandari hii ya Bagamoyo inatarajiwa kujengwa gati 9 huku kina cha Bandari ya Bagamoyo kwenda chini Mita 18.

Mr. Plasduce M. Mbossa amesema lengo la kupanua hizi Bandari ni kuweza kupokea meri kubwa, kuwavutia wawekezaji kwa wingi, kuondoa mlundikano wa mizigo bandarini na kuiwezesha serikali kupata kodi kwa wingi na kupatikana kwa ajira kwa Watanzania na kuwepo kwa usalama kwa kiwango kikubwa,

Mr. Plasduce M. Mbossa amewataka wanahabari pamoja na walili wa vyombo vya habari waendelee kushilikiana na TPA kwa ajili ya Maslahi mapana ya Taifa na waache kuandika habari za upotoshaji kwa jamii.

Habari Picha na Ally Thabiti


WAWEKEZAJI 58 KUTOKA NJE YA NCHI WAONYESHA NIA KUWEKEZA KATIKA KONGANI YA KAMAKA ILIYOPO MKOANI PWANI- KABENGULA


Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha.

WAWEKEZAJI 58 kutoka nje ya nchi wameonyesha nia ya kuwekeza katika kongani ya kisasa ya Modern Industrial Park -KAMAKA co.ltd iliyopo Disunyara, Mlandizi Kibaha mkoani Pwani .



Licha ya nia hiyo ya wawekezaji ,Kongani hiyo inaiomba Serikali kutupia macho changamoto ya barabara kwa kiwango cha lami kutokea Mlandizi ,huduma ya maji na umeme wa uhakika ili kuendelea kuvutia wawekezaji ndani na nje ya nchi ambao wakwenda kuomba kuweka ndani ya Kongani hiyo.

Hayo aliyaeleza Afisa Fedha na Masoko wa Turnkey Real Estate Tumaini Kabengula, kampuni ambayo inahusika na mauzo na masoko,na kuingia mkataba wa kutafuta wawekezaji kuwekeza viwanda kwenye viwanja 202 vilivyoko ndani ya Kongani ,kwa Waziri wa Viwanda ambae alifika kwenye eneo hilo kujionea changamoto zinazowakabili.

Alieleza, hadi sasa wawekezaji 58 wametembelea kongani na kuonyesha nia ya kuwekeza wakitokea nchi ya India, China ,Uturuki,Sudan ya Kusini ,Afrika ya Kusini ,Rwanda ,Somalia ,Tanzania , Pakistan,Yemen ,Zambia ,Falme za kiarabu ,Misri,Uganda ,Kenya na Canada.

"Mikataba iliyopo ni kumi ya ununuzi wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, pamoja na viwanja 24 vilivyoshikiliwa vikisubiri kusainiwa kwa mikataba."

Kabengula alieleza, wawekezaji watatu wamekwishaanza hatua za awali za ujenzi za ujenzi zinazohusisha michakato ya vibali vya mazingira (EIA) na michoro kwa ajili ya ujenzi na wanatarajia wengine watano waliosaini mikataba wataanza hatua za ujenzi mwaka huu.

Afisa huyo alifafanua kuwa, wawekezaji wengi ambao wameshaingia mikataba ya ununuzi wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa viwanda wangependa watakapoanza ujenzi changamoto hasa ya maji na umeme iwe imetatuliwa.

Hata hivyo ,alieleza miundombinu rafiki na wezeshi ndio kiungo pekee cha kuvutia wawekezaji zaidi.

"Tunaiomba Serikali kutatua hasa changamoto ya maji na umeme "alisisitiza Kabengula.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni utoaji wa vivutio vya kodi kwa kongani jirani na kutokuwepo vivutio hivyo katika kongani ya modern industrial park licha ya uwekezaji mkubwa uliofanyika na unaoendelea kufanyika kuna haribu ushindani wa haki wa kibiashara.

"Baadhi ya wawekezaji wanaamua kutokuchukua viwanja ndani ya Kongani kwa sababu ya kukosekana kwa vivutio vya kikodi kama ambavyo vinapatikana katika kongani jirani."

Kabengula alieleza, wawekezaji wengi wanakiri kuvutiwa na uzuri wa kongani ya modern industrial park lakini wanakwazwa na kutokuwepo kwa vivutio hivyo vya kikodi kama ambavyo vinapatikana kwenye kongani jirani.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alieleza ,kuhusu Changamoto ya maji alishaongea na waziri wa maji Jumaa Aweso na ameahidi kufika kwenye kongani hiyo kujionea uhalisia wa tatizo.

"Tunajivunia kuifungua Mkoa wa Pwani kwa ujenzi wa viwanda ,tuna kongani tatu na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Kongani 23 ,ambapo tunaishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuvutia wawekezaji na kuboresha na kuweka mazingira wezeshi hatua kwa hatua ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili "alieleza Kunenge.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji alieleza miundombinu wezeshi ni suala muhimu kwenye uwekezaji.

Kuhusu masuala ya kikodi alisema, watafuatilia ili kuona namna ya kuliweka sawa tatizo hilo.

"Ninashauri upande huo wa masoko ,waongeze taarifa ambazo hazipo kwenye taarifa ya mradi,wekeni wazi kila kitu hatua itakayosaidia ili ziwafikie wawekezaji kwa urahisi"alieleza Kijaji.

Nae Mkurugenzi Mtendaji, Mkandarasi Mkuu Afriq Engineering and Construction Co.Ltd mhandisi Charles Bilinga , alisema wamefikia asilimia 93 katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa miundombinu ambao utakamilika mwezi Februari mwaka huu .

Kongani ya KAMAKA ni mradi ambao ukikamilika utagharimu trilioni 3.5 kati ya fedha hizo bilioni 122.4 zitajenga miundombinu ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo hadi sasa sh .bilioni 35 zimetumika kwa ujenzi wa miundombinu na gharama zinazohusiana na uwekezaji huo.

CMSA YATINGA ZANZIBAR KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI

 


MWANDISHI WETU.


KATIKA kuadhimisha Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya dhamana (CMSA) imetinga visiwani humo kutoa elimu juu ya masuala ya Uwekezaji katika Masoko ya mitaji.

Maonyesho hayo ya 10 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar ambayo yanafanyika Dimani Fumba visiwani humo yameanza rasmi Januari 7, mwaka huu ambapo
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ally Mwinyi, atakuwa mgeni rasmi.

Akizungumza na wanahabari, Afisa uhusiano na elimu kwa umma, Stella Anastazi amesema, lengo kuu la kuja katika maonyesho hayo ni kutoa elimu juu ya masoko ya mitaji.

Stella amesema amefurahi kuona muitikio mzuri na mkubwa kutoka kwa watu mbalimbali waliotembelea banda la CMSA ili kujifunza.

 
"Nia na madhumuni ni kuleta elimu hii kwa wananchi wa Zanzibar, na pia kuwajuza maendeleo makubwa ambayo mamlaka imekuwa nayo mpaka sasa,"
Amesema imekuwa fursa kubwa kukutana na watu ambao wanaelimu juu ya mitaji hivyo hata kuwapa madini ya uwekezaji imekuwa rahisi tofauti na kukutana na mtu asiye na elimu ya masoko hayo.


Aidha Stella amesema ni wakati muafaka kwa wawekezaji kuwekeza kwani wao wanatoa ushauri zaidi na kujibu sintofahamu ambazo wananchi wamekuwa wakizipitia katika uwekezaji.


"Tumekuja na vipeperushi vingi vitazidi kumpa elimu muhusika ili kujua mambo mengi yanayohusu mitaji na masoko kupitia hivi vipeperushi pia vinampa mwongozo wa namna gani ya kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja na mambo mengi yanayofanyika CMSA,"amesema.

Aidha amewataka Watanzania kuwekeza ili kupata ongezeko la thamani ambayo ni faida kubwa sana kwao.

"Tuna kipeperushi kinacho toa elimu ya kujiepusha na uwekezaji wa upatu haramu ambao sio mzuri kwao maana akikosea anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria maana kuvunja sheria ya nchi ni kosa la jinai kufanya kosa hilo"amesema Stella.

Mmoja wa wananchi kisiwani Zanzibar Hamis Shaibu Hamad,amesema alikuwa akisikia mamlaka ya masoko ya mitaji lakini hakufahamu ni vitu gani vizuri vinapatikana huko ila baada ya kutembelea banda amefarijika kufahamu mengi.

"Unajua ukiwa haujapata elimu ya kitu husika unaweza kujikosesha fursa lakini mimi nimepata vitu vizuri kabisa kutika katika hili banda la CMSA nitakuwa balozi mzuri kwa wenzangu huko ili na wao waweze kuwekeza zaidi,"alisema Hamad.

Afisa uhusiano na elimu kwa umma kutoka CMSA, Stella Anastazi,akitoa elimu ya uwekezaji kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya biashara Zanzibar ( Zanzibar International Trade Fair)


Monday, 8 January 2024

MKURUGENZI MKUU MTENDAJI WA TRC AELEZA SGR ILIVYOKUWA NI RAFIKI KWA WENYE ULEMAVU


Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema mradi wa wa Treni ya Umeme (SGR) umezingatia maitaji ya msingi kwa watu wenye Ulemavu mfano kwa wasiona kuna alama maalumu kwa wenyeulemavu wa viungo miundo mbinu yao pia ni rafiki hivyo amewatoa hofu watu wenye ulemavu na wasiokuwa na ulemavu kwa usalama ni mkubwa katika mradi huu ukikamilika ametoa wito kwa jamii kuendelee kumuunga mkono Mh. Rais Samia Suluhu Hassani pia kumuombea kwa Mungu aendelee kuwa na hekma na afya tele huku Masanja Kadogosa akimpongeza Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuutekeleza mradi huu wa SGR.

Habri Picha na Ally Thabiti
 

WAZIRI WA UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI AWAFUNGULIA MILANGO WAJAPANI KUJA KUWEKEZA TANZANIA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mnyaa Mbarawa amewataka wajapani kuja kuwekeza Tanzania kwani Miundombinu ni rafiki kwa upande wa Bandari Barabara na Reli ambako kwa sasa mradi wa Treini ya Umeme umefikia Hatua Mzuri hivyo amewataka wajapani wajitokeze kwa wingi kuwekeza nae kwa upande wake waziri wa maliasili wa Japan amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani namna alivyotengeneza mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji.

Habari na Ally Thabiti

MKUU WA WILAYA WA DODOMA MJINI ATEKELEZA KWA VITENDO MAAGIZO YA RAIS SAMIA

Mh. Jabiri Shekimweri  Mkuu wa wilaya Dodoma Mjini amesema wanaendeleza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato, ujenzi wa Barabara za Tarula, Miradi ya Maji Madarasa na Barabara za Mzunguko Mh. Jabiri Shekimweri amesema pia wamejenga jengo la Machinga Complex ambako wamewezesha vijana kujiajili na kuwajili watu wengine, pia wanatoa pesa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ametoa wito kwa jamii waendelee kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani.

Habari na Ally Thabiti

Monday, 1 January 2024

HOSPITAL YA MKOA WA DODOMA YAMPONGEZA RAISI SAMIA

 Mganga mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Dodoma Dk. Ibezi Ernest amempongeza Raisi Dr. Samia Suluhu Hassani kwa kuweza kutengeneza miundombinu ya hospital ya mkoa wa Dodoma na kuweka vitanda vitatu na vitanda 28 vya wagonjwa mahututi nakufunga mtambo mkubwa wa kuzalisha gesi mitungi 300 kwa siku moja na kuweka vitanda 300 vya wagonjwa wanaotumia gesi pia Rais Samia aweza kununua mashine ya city scan ambayo inauwezo wa kuhudumia wagonjwa 3018 na kuweza kutengeneza maabara na kununua vitenganishi 86 na kununua gari la usimamizi moja pia kuna mpango wa m-mama lengo la mpango wa M-MAMA nikuweza kuwasaidia mama wajawazito pindi wanapoitahi kwenda kujifunngua magari yanawafuata walipo, Pia Rais Samia ameoa Ambulance Tatu kwaajili ya wagonjwa.

Dr. Ibenzi amesema hospital mkoa wa Dodoma inawahudumia watu wenye ulemavu pamoja na wazee bure pia inawataalamu wa lugha za alama kwenye watu wenye uziwi.

Ametoa wito kwa jamii wamuunge mkono Dr. Samia Suluhu Hassani















Habari picha na Ally Thabith