Wednesday, 10 January 2024

MKURUGENZI MKUU WA BANDARI AINISHA MIKAKATI MIZITO

 




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mr. Plasduce M. Mbossa amesema wameanza kazi za kutanua Bandari ya Dar es Salaam kwa kujenga Magati kuanzia namba 12 hadi 15 magati haya yanauwezo wa kupakia Meri kubwa pia watajenga vituo viwili vya mafuta pamoja na kujenga Mapipa ya kupakulia mafuta Mr. Plasduce M. Mbossa amesema eneo la kulasini EPZA itakuwa bandari kavu kwa ajili ya kuweka Contena kwa wingi, pia kutakuwa na maboya ya kuongozea Meri uku wakiongeza kina kwenye magati.

Huku ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo unaanza hivi karibu ambako wataanza kujenga magati mawili ambako gati moja gharama yake Bilioni Moja Mia Tatu Siti kila gati litakuwa na ulefu wa Mt 500 ambako gati moja linauwezo wa kupokea meri moja yenye uwezo wa kubeba Makontena elfu 25 bandari hii ya Bagamoyo inatarajiwa kujengwa gati 9 huku kina cha Bandari ya Bagamoyo kwenda chini Mita 18.

Mr. Plasduce M. Mbossa amesema lengo la kupanua hizi Bandari ni kuweza kupokea meri kubwa, kuwavutia wawekezaji kwa wingi, kuondoa mlundikano wa mizigo bandarini na kuiwezesha serikali kupata kodi kwa wingi na kupatikana kwa ajira kwa Watanzania na kuwepo kwa usalama kwa kiwango kikubwa,

Mr. Plasduce M. Mbossa amewataka wanahabari pamoja na walili wa vyombo vya habari waendelee kushilikiana na TPA kwa ajili ya Maslahi mapana ya Taifa na waache kuandika habari za upotoshaji kwa jamii.

Habari Picha na Ally Thabiti


No comments:

Post a Comment