Friday, 26 January 2024

TIGO YAENDELEA KUIMALISHA HUDUMA ZAO


Emmanuel Mfanyakazi wa Tigo amesema licha ya changamoto ya mvua zinazoendelea nchini Tanzania na kualibu miundombinu ya mawasiliano mfano kunduchi kusombwa kwa daraja na bomba kuondolewa na maji na mkongo wa mawasiliano kuondolewa na maji tigo imefanya maboresho kwa kujenga miundombinu ya mawasiliano na kulejesha 5G na data huku wakitengeneza njia moja ya mawasiliano na kuweka njia mbadara.

Bw. Emmanuel amesema kiasi cha Tilioni moja cha fedha kimewekwa kwaajili ya uwekezaji ndani ya Tigo na mpaka sasa kiasi cha fedha cha nusu yake kimetumika kwa Dar es Salaam na Zanzibar imefika 80% ya 5G ambapo Network yake imekamilika huku mikoa ya Mwanza, Tanga, Morogoro na Mikoa mingineyo kiwango cha 5G ni 50% huku jitihada zikihimalika kuboresha 5G vijiviji vyote hapa nchini.

Tigo walipata tenda kutoka serikalini 30% kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya mawasiliano Ndg Emmanuel amesema haya wakati wa kukabidhiwa tuzo na kampuni ya Ookla.

Nae kwa upande wake Bw. John kutoka Tigo amesema tigo imejitahidi kutoa huma iliyobora na yakisasa na kupelekea uchumi wa Tanzania kukua na uchumi wa mtu mmoja mmoja kukua kwa kasi ambako imepelekea watu kupata taarifa kwa kitekenolojia mfano Taarifa za kilimo, Uvuvi, Biashara na Sekta zinginezo.

Bw. John amewapongeza wateja wa Tigo Milioni 16 kwa kutumia huduma zao.

Habari na Vitoria Stanslaus

No comments:

Post a Comment