Kamshina Forodha Juma Hassani amesema katika siku ya kuhazimisha siku ya Forodha leo hii wanajivunia watu wanavyotoa ushirikiano wa kulipa kodi bila shuruti na kupelekea biashara Tanzania kukua na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi kubwa. Pia wameweka mfumo wa single window huku wakizibiti ungizwaji wa bidhaa haramu na feki na kwa upande wake kamishna wa TRA Alufayo Kidata amesema forodha inawezesha kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa fedha nchini Tanzania nae kwa upande wake mkuu wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Kamanda Jumanne Mulilo amesema wataendelea kuzibiti na kulinda mianya wa ungizwaji na utoloshwaji mizigo kwa njia za panya huku wakiendelea kuimalisha ulinzi na usalama kwa wawekezaji nae kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilala akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Edward Mpogolo amesema wafanya biashara wasiwe na tabia za kuleta migomo watumie njia za malidhiano huku akiwataka watumishi wa TRA kuwa na maadili mazuri.
Habarai Picha na Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment